YATIMA NCHINI TANZANIA WAFIKA MILION 2.4


Yatima nchini sasa wafikia milion 2.4

 WIZARA ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, imesema tafiti mbalimbali zilizofanyika zinazohusu watoto hapa nchini, zimeonesha kuongezeka kwa idadi ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi, wakati watoto yatima wakifikia milioni 2.4, imeelezwa.
Katika tafiti hizo, zimeonesha kuwa, tatizo la watoto wanaishi katika mazingira hatarishi limeonekana Mijini na Vijijini na kubwa zaidi kwenye Miji mikubwa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Tanga, Moshi, Dodoma na Mbeya.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Kijakazi Mtengwa, alisema hayo hivi karibuni wakati akiwasilisha mada yake iliyohusu Sekta ya Maendeleo ya Jamii kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Sekta hiyo uliofanyika hivi karibuni mjini Morogoro.
Alisema idadi ya watoto wanaishi mitaani imeendelea kuongezeka kutoka 1,579 mwaka 2007 hadi 2,010 mwaka 2011, wakati watoto 11,216 wanaoishi katika Vituo vya Kulelea Watoto kati yao 6,089 ni wavulana na 5,127 ni wasichana.
Pia alitaja idadi ya Watoto Yatima waliopo nchi nzima wamefikia 2,400,000 kati ya hao Wasichana ni 1,055,000 na Wavulana ni 1,345,000, ambapo idadi ya watoto 2,700 kati ya miaka 0-14 wanaishi na Virusi vya Ukimwi nchini.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo, sababu za watoto hao kuishi katika mazingira hatarishi, ni pamoja na umasikini katika familia, mifarakano na ukosefu wa amani kwenye familia na Wazazi kutowajibika katika malezi na makuzi ya watoto wao.
Hata hivyo, alisema sababu nyingine ni vitendo vya ukatili, udhalilishaji na unyanyasaji wa watoto kutoka kwa familia na jamii kwa ujumla, nyingine ni kufariki kwa Wazazi hasa kutokana na magonjwa mbalimbali, pia kuchangiwa na ndoa za umri mdogo pamoja na mimba zisizotarajiwa.

Comments

  1. Mi nafikiri kama walivyojitoa kujenga jengo la kusaidia wazee na yatima wafanyiwe hivyo na watu wengine tuige mfano wa kusaidia wengine.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

WATOTO WA MITAANI NA JINSI YA KUWASAIDIA

AYA ZA BIBLIA KUHUSU WATU WENYE ULEMAVU

TUWAKUMBUKE WATOTO WENYE MTINDIO WA UBONGO KAMA KUNDI MAALUM KATIKA JAMII ZETU