Posts

TUWASADIE WATOTO YATIMA NA WATOTO WA MITAANI

Image
                                              Hiki ndicho kitanda cha mtoto huyu                                                                                Kwa watoto hawa popote ni kitanda    Wapo watoto wengi ambao wanaishi maisha ya shida na taabu nyingi, wengi wakiwa wameondokewa na wazazi wao (wamefiwa na wazazi wao). Ni kweli kuwa serikali ina jukumu la kuwa...

WATOTO WA MITAANI WANASWA KITUO KIKUU CHA MABASI UBUNGO, WAFIKISHWA MAHAKAMANI DAR-ES-SALAAM

Image
Watoto wa mitaani wakipelekwa kwenye gereza la watoto lililopo Kisutu jijini Dar es Salaam. WATOTO wa mitaani  leo wamepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Sokoine Drive jijini Dar na kufunguliwa mashitaka ya uzururaji. Watoto hao walinaswa kwenye msako uliofanyika kwenye kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani ‘Ubungo Bus Terminal’. Pichani juu ni baadhi ya picha za watoto hao na yeyote anayetaka kujua zaidi kuhusu watoto hao, afike kwenye gereza la watoto lililopo Kisutu.  Majina yao yapo kwenye karatasi hapo juu.   SERIKALI ITAFUTE NJIA MBADALA YA KUWASAIDIA HAWA WATOTO, HII KAMATAKAMATA SIO SULUHISHO LA KUONDOKANA NA WATOTO WA MITAANI NA OMBAOMBA KWA UJUMLA, KUTOKANA NA FURSA TULIZONAZO NCHINI NI VEMA SERIKALI IKATENGA ENEO MAALUMU KWA AJILI YA HAWA WATOTO, PIA SERIKALI IWAWEZESHE KWA NAMNA AMBAYO ITAWAFANYA WAONDOKANE NA UTEGEMEZI NA KUOMBAOMBA, KWA MFANO WALE WENYE VIPAJI KUWAENDELEZA KATIKA VIPAJI VYAO NA WENGINE WAPEWE NYEZO ZA KUJITEGEMEA KAMA ...

WAFANYAKAZI WA BENKI YA NBC WATEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA NA KUWAKABIDHI MISAADA.

Image
 Wafanyakazi wa Benki ya NBC kitengo cha operesheni, wakipozi kwa picha na watoto wanaolelewa katika kituo cha Ijango Zaidia Orphanage cha Sinza walipokwenda kupeleka msaada wa vyakula, sabuni, mafuta ya kupikia na vyandarua ikiwa ni moja ya mikakati ya NBC kurudisha sehemu ya faida waipatayo katika jamii. Hafla ilifanyika kituoni hapo jijini Dar es Salaam juzi. Wengine ni watumishi wa kituo hicho.  Mkurugenzi wa Uendeshaji na Huduma wa Benki ya NBC Tanzania, Cornie Loots (kulia) akikabidhi msaada wa vyakula, mafuta ya kupikia, sabuni na vyandarua kwa Mkuu wa kituo cha watoto yatima cha Ijango Zaidia Orphanage , Bi. Zaidia Nuru Hasani, vilivyotolewa na NBC kituoni hapo, Sinza, Dar es Salaam juzi.  Mtoto anayelelewa katika kituo cha watoto yatima cha Ijango Zaidia Orphanage, Ramia Mahmoud , akipokea mafuta ya ngozi kwa niaba ya wenzake vyaliyotolewa msaada na Benki ya NBC kutoka kwa mfanyakazi wa benki hiyo, Ernest Paulo Mbepera (kulia) kituoni hapo, Sinz...

'''LIFE WITHOUT LIMIT'''

Image
Nick Vijicic alizaliwa 1982 Mwezi wa kumi na mbili, huko Serbian Melbourne, Astralia kama mlemavu asiyekuwa na miguu wala mikono,mwili wake upo kama nusu mtu. Siku alipozaliwa wazazi wake walilalamika sana na muda mwingine walijuta kumzaa mtoto huyo, hata katika kanisa alilokuwa akiongoza Baba yake lilimtatiza sana kiasi ambacho alikosa raha ya kutetea yaliyotokea kutokana na imani aliyokuwa nayo.                                                  Nick Vijicic. Wazazi wa Nick walikuwa wakijuta kila siku na hata kutubu kwa Mungu kwa kudhani wamemkosea Mungu kuwaletea mtoto huyo.Walijiuliza kwa nini imetokea? Na nikosa la nani? Na walikuta kuwa si madaktari wala mimba ya mama yake kama kosa la kusababisha kuwa jinsi alivyo. Maisha yakiwa ma...
Image
“”””””””””HA KUNA UGUMU WOWOTE   KUFUNDISHA WATOTO VIZIWI “ Asema mwalimu-mwanafunzi   Madeghesho Fabiola. Watu wengi   huwa na notion kwamba kufundisha watoto viziwi ni kitu kigumu sana hasa ukizingatia kuwa wanahitaji lugha ya alama kufundishiwa, kwa mwalimu Fabiola anaona si changamoto kubwa kama tunavyofikiri hivyo kuwaasa waalimu wengine wasiogope kujifunza lugha ya alama ili kuwasaidia watoto hawa. Mwalimu Fabiola ambaye anachukua shahada ya awali ya elimu maalumu kitengo cha viziwi katika chuo cha kumbukumbu cha Sebastian Kolowa kilichopo Lushoto   mkoani Tanga, ameyasema haya baada ya kumaliza mafunzo ya vitendo (field) aliyokuwa akiyafanya katika shule ya msingi Meru iliyopo mkoani Arusha, ambayo shule hiyo imeambatana na kitengo cha viziwi. Mwalimu huyo aliongeza kuwa “Nimejisikia fahari kubwa sana kuweza kuwasiliana na watoto hawa na kuelewana nao vizuri, ni watoto ambao kwa kweli wanafundishika na wana shauku kubwa ya kujua vitu...

UHABA WA WALIMU WA LUGHA ZA ALAMA WAKWAMISHA VIZIWI KUPATA ELIMU.

Image
Wanafunzi wa Shule ya Viziwi Dongobesh  wakiimba wimbo wa Taifa shuleni hapo mkoani Manyara. Kukosekana kwa walimu wa kufundisha lugha ya alama, imesababisha wanafunzi 39 kati ya 40 wenye ulemavu wa kutosikia waliomaliza elimu ya sekondari mwaka jana kupata daraja la sifuri.   Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Jasmine-Angellah Kairuki, amesema kukosekana kwa walimu wa kufundisha lugha ya alama, imesababisha wanafunzi 39 kati ya 40 wenye ulemavu wa kutosikia  waliomaliza elimu ya sekondari mwaka jana kupata daraja la sifuri. Akizungumza Dar es Salaam juzi, Kairuki alisema changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu huo kwa elimu ni kutokuwa na fursa sawa ya kutumia lugha wanayomudu. Alisema utoaji elimu kwa watu wenye ulemavu huo, hauridhishi kutokana na walimu waliopo kuwa wachache ndiyo maana wanafunzi 39 walifeli na mmoja kupata daraja la nne. “Tatizo hili linatokana na walimu  wanaofundisha lugha ya alama kuwa wachahe, hivyo nakuagiza Kamishn...

"JENGENI MOYO WA HURUMA, UPENDO NA UVUMILIVU KWA WATOTO WENYE ULEMAVU"!

Kituo cha Watoto Walemavu cha Siuyu, Jimbo Katoliki Singida, kilizinduliwa rasmi na Askofu Desiderius Rwoma wa Jimbo Katoliki Singida, kunako tarehe 20 Februari, 2007. Kituo hiki kinahudumiwa na muungano wa Shirika la Wamissionari wa Pallotini pamoja na Watawa wa Pallotini pamoja na waamini walei, wanaopenda kumwilisha karama ya Mtakatifu Vincenti wa Palloti katika maisha yao ya Kikristo.   Wamissionari hawa wanashirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha kwamba, watoto wenye ulemavu wanaonjeshwa kwa namna ya pekee, ile Injili ya Upendo kutoka kwa Kristo mwenyewe. Wengi wa wafanyakazi katika kituo hiki ni watu wa kujitolea, lakini walau kila mwezi, wanapata ruzuku kidogo kama alama ya shukrani kwa mchango wao kituoni hapo. Jumla ya Euro 90,000 zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa kituo hiki, mchango kutoka kwa Wasamaria wema. Vatican kwa upande wake, imechangia kiasi cha Dolla za Kimarekani 15, 000. Kituo cha walemavu Siuyu, Jimbo Katol...