MIUNDOMBINU YA SHULE NI KIKWAZO KWA WATOTO WENYE ULEMAVU KUPATA ELIMU MUSOMA
Rajabu Josephat mwanafunzi mwenye ulemavu wa viungokatika shule ya Msingi Nyankanga na Pius Ligamba wa shule ya Secondary Kemoramba. |
Pius Ligamba Mwanafunzi wa shule ya msingi Kemoramba wilayani Musoma |
Shule ya sekondari Kemoramba, Shule ya msingi Nyankanga na
Shule ya msingi Mmahare ni baadhi ya
shule zilizotembelewa na kuonekana hazina miundombinu ya majengo rafiki ili
kuwezesha wanafunzi wenye ulemavu kusoma bila matatizo makubwa.
Shule nyingi wilayani musoma vijijini hazina majengo yenye
kujali mahitaji ya walemavu wa viungo wala hawana mipango ya karibuni ya kutengeneza
miundombinu kwaajili ya walemavu.
Mkazi mmojawapo wa kijiji cha Nyankaga bwana Mr Wekesa Nyamarwa, alimwambia mwandishi wa habari hii kuwa mototo
wake ambaye ameshapitisha umri wa kwenda shule alichagua kutokumuandikisha ili
kumuepusha na mazingira hatarishi na mabaya ambayo anasema yasingemuwezesha mtoto
wake kufuatilia vyema masomo yake.
Bwana Nyamarwa anajua mtoto wake atapata matatizo makubwa akiwa shuleni na katika masomo yake ambayo yatamchanganya na kumfanya aache shule bila kufikia malengo yake aliyojiwekea.Alitoa mfano wa shule ya msingi Nyakaga kuwa haina miundombinu inayoweza kumfanya mlemavu ajisikie nae kama wanafunzi wengine.
Bwana Nyamarwa ameendelea kueleza kuwa idadi ya wanafunzi
wenye ulemavu wanaosoma shule ni ndogo zaidi ya wale walio majumbani na ambao
hawasomi ingawa wana umri wa kwenda shule, na kuwa majingira mabovu ndicho
chanzo cha wanafunzi wengi wenye ulemavu kushindwa kwenda klujiandikisha shule.
Wanafunzi walemavu wa viungo wanapata changamoto hasa
nyakati za kwenda chooni ambapo vyoo vimejengwa bila kuzingatia mahitaji yao
kwani I nawalazimu kutembea juu ya majo machafu ya chooni kabla ya kufika
kwenye shimo la choo.Pia madarasa hayajajengwa kuzingatia mahitaji ya walemavu.
Nchi ina safari ndefu katika kufikia lengo lake la kuwa na
elimu inayofikiwa na watoto wote.hii ni changamoto kwa siyo tu mamlaka ya
halmashauri ya Musoma bali serikali yote kwa ujumla katika kufikia mahitaji ya
kujifunzia/kusomea kwa watoto wa kada zote pasina kujali hali ya mwanafunzi
husika mpaka kufikia mwaka 2025.
Comments
Post a Comment