SERIKALI INAYATAMBUA HAYA.?
Adha, shida na mateso wanayoyapata watoto katika maeneo ya machimbo ya dhahabu Chunya.
Mkazi
wa kijiji cha Chang'ombe, Kata ya Mkwajuni jimbo la Songwe Mbuke Kulwa
akitafuta dhahabu katika mto mara baada ya kufukuzwa na mumewe ambaye
alidai kuwa anaishi na mke mwingine, huu ni sehemu ya ukatili wa Kijinsia
ambao Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA kimekuwa kikipinga
na kukemea katika harakati zake za kupinga ukatili wa Kijinsia.
Kijana huyu Mwanafunzi wa shule ya Msingi Mkwajuni aliyejitambulisha
kwa jina la Asajile mkazi wa kitongoji cha Kamficheni Jimbo la Songwe
Mkwajuni wilayani Chunya akitafuta dhahabu ili aweze kujikimu kutokana
na mahitaji muhimu ya kila siku, Asajile ni miongoni mwa vijana wengi wa
shule za Msingi ambao wamekuwa wakiacha masomo kwa na kwenda katika
machimbo ya dhahabu wilayani Chunya.
Watoto hawa wakazi wa kitongoji cha Kigamboni kilichopo Jimbo la Songwe
wilayani Chunya wakitafuta maji kwa ajili ya matumizi ya kila siku
kutokana na uhaba wa maji katika mji huo,familia nyingi wilayani Chunya
zimekuwa zikihangaika kusaka maji safi na salama kutokana na kukosekana
mabomba ya maji kutosheleza kaya jimboni humo.
Mtoto
huyu ambaye hakutambulika jina lake akiokota dhahabu ili kujipatia
kipato kutokana na hali ngumu ya maisha yanayowakabili wakazi wa jimbo
hilo.
Comments
Post a Comment