Mungu ni mwaminifu sana. Hawa watoto ni walemavu wa akili wapo shule ya msingi Milongo ya jijini Mwanza, pamoja na ulemavu wao ila wana vipaji vya ajabu sana. Katika maisha yangu wameweza kuniondolea ule mtazamo kuwa walemavu hawawezi jambo lolote katika maisha Yao, huyo binti ana kipaji cha uimbaji, na hao vijana wana vipaji mbalimbali kama vile kucheza mpira yote hiyo ni katika kuutambua ukuu wa Mungu. Sio hao tuu kuna mifano mbalimbali ya Watu wenye ulemavu na wana vipaji mbalimbali mfano Voice wonder mwimbaji kipofu wa Marekani, Lena Maria. Dada mlemavu wa viungo wa Sweden mwimbaji mzuri sana na wengine wengi, hiyo ni mifano michache katika kuthibitisha kuwa ulemavu si kutokuweza.
SIMULIZI YA KWELI
Nililazimika kulala kwenye mitaro ili niweze kuiona kesho Miaka takribani saba iliyopita kwenye mtaa fulani hapa Njombe katika usiku wa giza zito uliofunikwa na baridi kali iliyochangamana na ukungu, wapo vijana kadhaa wamelala chini ya mitaro, wamesogeleana karibu ili angalau wapate joto katika miili yao. Mashuka yao ni maboksi yaliyotolewa vitu vya thamani na kutupwa jalalani. Kati ya vijana hawa ambao wamelala chini ya moja ya mitaro ya mji huu wa Njombe yupo kijana aitwaye John Mwingira ambaye kabla ya miaka saba iliyopita alikuwa akiishi nyumbani kwao Ifakara, wilayani Kilombero mkoani Morogoro. Huko alikuwa akiishi na wazazi wake wote wawili, lakini baadaye wazazi wake waliachana kufuatia kutokuwepo maelewano baina yao. Baba yake akahamia Njombe na mama yake akabakia Ifakara. “Baada ya wazazi wangu kuachana maisha yalikuwa magumu pale nyumbani Ifakara hivyo mama akanishauri nimfuate baba hapa Njombe, nilifika Njombe na kuonana na baba yangu am...
Comments
Post a Comment