Posts

ABOUT ME

Image
FULL NAME  SANJI MIRUMBE JAMES EDUCATION Bachelor of education in special needs PROFESSIONAL. Specialist teacher Why I decide to create this blog. First of all I thank God for who I am, I thank Him for his love and for this case I think it is my time now to return to God what He gave me. What I always walk with, is divine law of God that is law of love, that “you shall love God at the same time love others” and another is golden law that “do to others things that you want them to do to you. Why am I saying this? You see these days there is a lot of suffering and miseries many inhuman practice to vulnerable children, they are helpless and they need someone to her their voice, why should I think of them? It is because God did it to me at a first time, so now it is my time to return the favor. JOHN: 13:15:1  have set you an example that you should do as I have done for you. From this fact I made this blog for the vulnerable children to be the voice of the voic...

KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALEMAVU KITAIFA IRINGA , SERIKALI YA TANZANIA YAPIGA MARUFUKU UJENZI WA MAJENGO YASIYO RAFIKI NA WALEMAVU.

 SERIKALI  imeziagiza  mamlaka  za  usafiri  wa majini na nchi kavu (SUMATRA )  nchini  kuanza mchakato  wa  kukaa na  wamiliki wa  vyombo  hivyo  ili kuanza  uangizaji  wa vyombo  vya usafiri yakiwemo mabasi ambayo ni  rafiki na walemavu nchini huku ikipiga marufuku  majengo ya   serikali kujengwa bila kuwepo kwa  mchoro  unaoonyesha mazingira yanayozingatia makundi  yote ya jamii  likiwemo la walemavu wa viungo . Agizo   hilo  limetolewa na  waziri  mkuu Mizengo  Pinda wakati  wa maadhimisho ya  siku ya  walemavu  duniani yaliyofanyika   kitaifa  katika  viwanja  vya kichangani mkoani  Iringa jana. Akiwahutubia   walemavu hao na  wananchi  waliofika katika  viwanja   hivyo waziri  mkuu ,aliyewakilishwa na waziri  wa nchi  ofi...

SHULE YA WALEMAVU BUHANGIJA JUMUISHI YAELEMEWA NA CHANGAMOTO

Image
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akimsikiliza kwa makini Mkuu wa kitengo cha watoto walemavu shule ya msingi Buhangija Jumuishi ya mkoani Shinyanga Mwl. Loyce Daudi aliyekuwa akimwelezea changamoto mbalimbali walizonazo shuleni hapo.(Picha na Zainul Mzige). Na MOblog, Shinyanga SHULE ya watoto wenye ulemavu ya Buhangija Jumuishi inakabiliwa na changamoto kubwa zinazofanya maisha kwa watoto hao kuwa magumu. Miongoni mwa changamoto hizo ni kukosekana kwa huduma za matibabu, walimu wa kutosha na mabweni. Hayo yamebainika wakati wa ziara fupi ya Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues. Mkuu wa Kitengo cha watoto walemavu shule ya msingi Buhangija Jumuishi iliyopo mkoani Shinyanga Mwl. Loyce Daudi, ndiye aliyeelezea ugumu uliopo katika shule hiyo yenye wanafunzi 209 wenye ulemavu w...

UJUMBE WA SIKU YA WALEMAVU DUNIANI.

  Ikiwa zimebaki takribani siku saba kabla ya kuadhimisha siku ya walemavu Duniani, kuna maswali mengi ya kujiuliza kama jamii tunayozungukwa na watoto pamoja na watu wazima wenye ulemavu wa aina tofauti tofauti, moja ya maswali hayo ni kama ifuatavyo, umeifanyia nini jamii ya watu wenye ulemavu,? umeguswa kwa namna gani na hali zao,? umekuwa ni mtu unaezidi kupotosha ukweli kuhusu ulemavu au ni mtu unayesaidia kuondoa mitazamo hasi dhidi ya watu wenye ulemavu? Je unawasaidia walemavu kwa kuwa unawahurumia au ni kwa sababu ni jukumu lako? sambamba na maswali mengine mengi na majibu tofauti tofauti, jambo moja la msingi ni kutathimini kwa kina ukuu na uweza wa Mungu kwa kila jambo, tofauti zetu zisitufanye tukadharauliana nakutokuthaminiana. Jambo la msingi tunapokaribia kuadhimisha siku ya walemavu Tanzania, ni kuhakikisha tunakuwa na upendo kwa watu wenye ulemavu tukiwachukulia ni sehemu muhimu ya jamii yetu, tushirikiane nao katika mambo mablimbali ya kijamii na kiuchumi kwa k...

TANZANIA: MAISHA YA HATARI YA WATOTO WACHIMBA DHAHABU

Image
Vijana wadogo wakike na wakiume wa Kitanzania wanashawishika kujiingiza katika uchimbaji wa dhahabu wakitumaini kupata maisha bora, lakini baadae wanajikuta wamekwama katika mzunguko mbaya wAa hatari na kukata tamaa. Tanzania na wahisani wanahitaji kuwatoa watoto hawa katika migodi na kuwaingiza shuleni au katika mafunzo ya ufundi stadi. Janine Morna, mtafiti wa haki za watoto wa shirika la Human Rights Watch (Dar Es Salaam) – Watoto wenye umri mdogo wa hadi miaka minane wanafanya kazi katika migodi midogo midogo ya dhahabu ya Tanzania, ikiwa na hatari kubwa kwa afya zao na hata maisha yao, shirika la Human Rights Watch imesema katika ripoti iliyotolewa leo. Serikali ya Tanzania inapaswa kukomesha ajira kwa watoto katika uchimbaji mdogo mdogo wa dhahabu, ikiwa ni pamoja na katika migodi isiyo rasmi, na isiyo na leseni, na Benki ya Dunia na nchi wahisani wanapaswa kuunga mkono juhudi hizi. Ripoti yenye kurasa 96, “Kazi ya Sulubu yenye Sumu: Ajira kwa Watoto na...

AJIRA ZA WATOTO MIGODINI NCHINI TANZANIA ZINA ATHARI MBAYA

Image
  Shirika la Kuteteta Haki za Binadamu la Human Rights Watch limetangaza kuwa, watoto wa maeneo ya migodi nchini Tanzania wanakabiliwa na  mazingira magumu.   Ripoti ya shirika hilo inabainisha kwamba, watoto wamekuwa wakijiingiza kwenye ajira ya uchimbaji madini nchini Tanzania huku wengi wao wakiathirika kiafya. Aidha ripoti ya Shirika la Kuteteta Haki za Binadamu la Human Rights Watch imesema kuwa, kuna vitendo vya dhuluma na ukatili wa kijinsia unaofanywa dhidi ya watoto hao wanaofanya kazi katika baadhi ya maeneo ya migodi nchini Tanzania. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, baadhi ya watoto hao wapo hatarini kuangukia kwenye matatizo ya kiafya, ikiwamo mtindio wa ubongo kutokana na  kemikali zinazopatikana kwenye machimbo hayo ya madini. Idadi kubwa ya watoto hao hufanya kazi kwenye mazingira magumu na wakati mwingine hulazimika kuingia kwenye mapango yaliyopo chini kwa chini, kwa ajili ya kusaka madini, imebainisha ripoti hiyo ya Human Rights Watch.