Posts

UNYANYAPAA UNAVYOTUMIKA KUWANYIMA FURSA WATU WENYE ULEMAVU.

Na Francis ole Rikanga. TAFSIRI ya neno ulemavu hutofautiana kutoka kwa mtaalam moja hadi mwingine, kutokana na mazingira ambamo tafsiri hiyo hutumika. Baadhi ya wataalam hutafsiri kuwa ulemavu ni ukosefu wa viungo muhimu katika mwili wa binadamu na wengine husema ulemavu ni ukosevu wa fikra. Pamoja na watalaam na watu mbalimbali katika jamii kutofautiana, Bw.Fredy Msigallah ambaye ni Afisa mtetezi wa Haki za watu wenye Ulemavu kutoka CCBRT anasema ulemavu ni kukosekana au kuwepo kwa ukomo fursa ya kushiriki katika maisha ya kijamii kwa kiwango sawa na watu wengine kwa sababu za kimaumbile, kiakili na kijamii. Kwakwe ulemavu si ukosefu wa viungo bali ni ukosefu wa fursa ya kushiriki katika maisha ya jamii kunakosababishwa na vikwazo vya mazingira, kimtizamo na mfumo uliopo ndani ya jamii. Ni ukweli usiopingika kuwa licha ya kuwepo kwa vikwazo bado kuna watu wenye ulemavu waliodhihirisha kuwa ulemavu sio viungo. Ipo mifano hai ya watu wenye ulemavu iwe ya viungo, kuona...

Muone MTU si ULEMAVU ALIONAO.

Image
MUONE MTU NA SI ULEMAVU WAKE, Ni maneno machache sana ila yana maana kubwa sana miongoni mwetu, siku zote tunauona ulemavu na kujiuliza huyu mlemavu anaweza kufanya jambo gani? Binadamu wote ni sawa ulemavu ni tofauti za kimaumbile tu ila vipawa na karama Mungu alizomgawia kila mmoja zinabaki kuwa ndani ya mtu na si ndani ya ulemavu mtu alionao.  Katika kuthibitisha kauli yangu kuna mifano mingi sana ya watu wenye ulemavu waliofanya mambo makubwa tu kuliko watu wasio walemavu, mfano watu Kama Voice wonder, Lena Maria, hawa na wengine wengi wameushangaza ulimwengu kwa sauti zao nzuri Mungu alizowajalia achilia mbali ulemavu walionao. Ni vizuri tukamtazama mtu na si ulemavu alionao. Hiyo itatusaidia sana kuwathamini na kuwajali sana watu wenye ulemavu na hiyo itapelekea kuwapa fursa sawa na watu wasio na ulemavu.

HUU NI MFANO WA KUIGWA NA WANAJAMII WENGINE.

Image
Mh. Kamani ajenga kituo cha kutunza walemavu wa ngozi NA PETER KATULANDA, BUSEGA. VITENDO vya mauaji ya kikatili kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) wilayani Busega, vimemsukuma Mbunge wa jimbo la Busega mkoani Simiyu, Dk Titus Kamani, kuanzisha ujenzi wa kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu huo. Kituo hicho kinachojengwa Kijiji cha Lukungu, Kata ya Lamadi, kitakachokuwa na uwezo wa kuchukua watoto zaidi ya 100, kitagharimu zaidi ya sh Bilioni 1.5. Kutokana na jitihada za Mbunge huyo kuokoa maisha ya walemavu hao, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, amemuunga mkono kwa kuchangia kiasi cha sh milioni 5 kwa ajili ya kuongeza nguvu ya ujenzi ambao tayari umeanza na unatarajiwa kukamilika Agosti mwaka kesho. Akizungumza katika eneo la ujenzi huo ambao umefikia hatua ya msingi jana, Dk Kamani alisema “Katika vitu ambavyo navifikiria sana na ningependa niondoke madarakani nikiwa nimevikamilisha, ni pamoja na kituo hiki cha walemavu.”   “Hapa sisikilizi la mtu lazima kit...

ASILIMIA 90 YA WATOTO WALEMAVU HAWAENDI SHULE KUTOKANA NA DHANA POTOFU KATIKA JAMII MIMI NA WEWE TUSAIDIANE KUWATETEA WALEMAVU

Serikali imeombwa kulipa kipaumbele suala la umuhimu wa makundi ya walemavu kupewa haki zao za msingi ikiwemo elimu kufuatia utafiti uliofanywa na wataalama wa kimataifa wanaohudumia walemavu wa aina tofauti nchini kubaini kuwa asilimia 98% ya makundi ya watoto wenye ulemavu hawaendi shule kwa sababu mbali mbali ikiwemo dhana potofu iliyopo miongoni mwa jamii.  Akizungumza na mamia ya wananchi katika kijiji cha Duga kilichopo kata ya Duga wilayani Mkinga katika zoezi la kuhamisisha jamii kuwapatia haki zao za msingi walemavu  mtaalam wa kuhudumia walemavu kutoka nchini Thailand Dr,Kirsi Salo  amesema katika utafiti wao walioufanya katika mikoa mbali mbali nchini baadhi yao wamefichwa majumbani kutokana na imani haba za kishirikina  kuwa kuzaa mtoto mlemavu ni mikosi ndani ya familia na baadhi ya familia hudiriki hata kupoteza maisha yao. Kwa upande wake kiongozi wa kanisa la kilutheri usharika wa Duga mchungaji Clementi Hongele ambaye amedai ...

SIKU YA MTOTO WA AFRIKA

Image
Siku ya Mtoto wa Afrika na Elimu bora isiyo vikwazo Mtoto akitafakari Juni 16 ya kila mwaka Umoja wa Afrika sambamba na washirika wake husherekea siku ya mtoto wa Afrika- au kwa kimombo Day of African Child (DAC ), ikiwa ni kumbukumbu ya mwaka 1976 ambapo waandamanaji wanafunzi wa shule za Soweto Afrika ya Kusini waliandamana kupinga elimu iliyokuwa inatolewa kwa manufaa ya utawala wa kibaguzi wa makaburu. Maandamano hayo yalipokelewa na mikono usio na huruma na masikio yasiyo sikivu ya utawala wa kibaguzi na kusababisha vifo vya mamia ya wanafunzi “Watu wangu, leo nipo huru nipo huru kwa kuwa sintosahaulika kabisa, siku itatimia ambapo kila mmoja wetu atakuwa huru, huru kutokana na unyanyasaji, huru kutokana na uwoga, huru kutokana na kuuwawa, nyinyi ni vijana wadogo mtaishi hadi kuiona siku hiyo na ata kama sintofanikiwa kuiona siku hiyo nyinyi mnatakiwa kusadiki tu kuwa nitakuwepo siku hiyo, hapa ni nyumbani kwangu, pahala pangu pa kuishi.” Hayo ni ...

AJIRA KWA WATOTO NI ZAO LA UBEPARI.

Image
Tarehe 12 Juni ya  kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ajira kwa Watoto. Katika maadhimisho haya hufanyika makongamano na hafla mbalimbali kujaribu kupiga kampeni dhidi ya ajira za watoto. Tanzania ni miongoni mwa nchi 174 zilizoridhia azimio namba 182 la kukomesha utumikishaji watoto chini ya umri wa miaka 18.  Hakuna anayepinga  juu ya kuwepo ajira za watoto kila mahala. Kwa mfano, kwa mujibu wa uchunguzi wa gazeti la  Mwananchi kupitia mradi wa kupambana na ajira ngumu kwa watoto Zanzibar,  zaidi ya watoto 15,000  ndani ya Zanzibar wanajishughulisha na ajira tena zile ngumu. http://www.mwananchi.co.tz/habari/habari-ya-ndani/Ajira-ngumu--kwa-watoto-Zanzibar/-/1724700/2074082/-/3uj83s/-/index.html Aidha, kuna vilio kama hivyo vya ajira za watoto pia Tanzania  Bara hususan  katika maeneo ya machimbo ya migodini yakiwemo Mererani mkoani Manyara, maarufu kwa uchimbaji wa madini aina tanzanite. http://www.bbc.co.uk...

TAREHE 12/06 KILA MWAKA TUIKUMBUKE SOTE, TUPIGANIE HAKI ZA WATOTO WALIO KATIKA AJIRA MBAYA.

Image
Siku ya kimataifa ya kupinga ajira ya watoto: Ajira na dhuluma za kimapenzi ndio jinamizi kubwa zaidi.   Kila mwaka Juni 12 ni siku ya kimataifa ya kupinga ajira kwa watoto na mwaka huu kauli mbiu ni "funga bao kutokomeza ajira ya watoto". Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF katika kuadhimisha siku hiyo imetoa wito wa hatua za haraka kuchukuliwa kote duniani ili kukata mirija ya ajira mbaya ya watoto. UNICEF pia inasherehekea miaka kumi ya ushirikiano na shirika la IKEA katika kulinda haki za watoto na kupambana na ajira ya watoto. UNICEF inasema dola milioni 190 zilizotolewa kwa ushirikiano zimebadili maisha ya watoto wapatao milioni 100 katika nchi 30 na hivyo kuifanya UNICEF na IKEA kuwa wahisani wakubwa. Wataalamu wawili wa Umoja wa Mataifa kuhusu utumwa na kuuzwa kwa watoto wamesema kuwa zaidi ya watoto milioni 215 wanafanya kazi kote duniani huku zaidi ya nusu yao wakipitia hali ngumu zikiwemo dhuluma za kimapenzi na za kikazi. Aki...