TAREHE 12/06 KILA MWAKA TUIKUMBUKE SOTE, TUPIGANIE HAKI ZA WATOTO WALIO KATIKA AJIRA MBAYA.

Siku ya kimataifa ya kupinga ajira ya watoto: Ajira na dhuluma za kimapenzi ndio jinamizi kubwa zaidi.

 

Kila mwaka Juni 12 ni siku ya kimataifa ya kupinga ajira kwa watoto na mwaka huu kauli mbiu ni "funga bao kutokomeza ajira ya watoto".
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF katika kuadhimisha siku hiyo imetoa wito wa hatua za haraka kuchukuliwa kote duniani ili kukata mirija ya ajira mbaya ya watoto.
UNICEF pia inasherehekea miaka kumi ya ushirikiano na shirika la IKEA katika kulinda haki za watoto na kupambana na ajira ya watoto. UNICEF inasema dola milioni 190 zilizotolewa kwa ushirikiano zimebadili maisha ya watoto wapatao milioni 100 katika nchi 30 na hivyo kuifanya UNICEF na IKEA kuwa wahisani wakubwa.

Wataalamu wawili wa Umoja wa Mataifa kuhusu utumwa na kuuzwa kwa watoto wamesema kuwa zaidi ya watoto milioni 215 wanafanya kazi kote duniani huku zaidi ya nusu yao wakipitia hali ngumu zikiwemo dhuluma za kimapenzi na za kikazi. Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga ajira ya watoto mjumbe maalum kuhusu utumwa Gulnara Shahinian amesema kuwa moja ya ajira za watoto zinazotajwa kwa sasa ni pamoja na kwenye migodi ambapo hadi watoto wa umri wa miaka mitatu hufanya kazi.  

Kulingana na maoni yake Shahinian anasema kuwa ni lazima serikali zitekeleze majukumu yao ya kulinda na kuwarejesha kwenye maisha ya kawaida waathiriwa wa ajira ya watoto , kuwafikisha mbele ya sheria wahusika na kuliangamiza kabisa tatizo hilo. Katika mataifa mengi ya Afrika, watoto huajiriwa kama wafanyakazi wa nyumbani, ambako wengi wao hukumbwa na dhuluma mbalimbali, zikiwemo dhuluma za ngono.

Comments

Popular posts from this blog

WATOTO WA MITAANI NA JINSI YA KUWASAIDIA

TUWAKUMBUKE WATOTO WENYE MTINDIO WA UBONGO KAMA KUNDI MAALUM KATIKA JAMII ZETU

AYA ZA BIBLIA KUHUSU WATU WENYE ULEMAVU