Posts

ASILIMIA 90 YA WATOTO WALEMAVU HAWAENDI SHULE KUTOKANA NA DHANA POTOFU KATIKA JAMII MIMI NA WEWE TUSAIDIANE KUWATETEA WALEMAVU

Serikali imeombwa kulipa kipaumbele suala la umuhimu wa makundi ya walemavu kupewa haki zao za msingi ikiwemo elimu kufuatia utafiti uliofanywa na wataalama wa kimataifa wanaohudumia walemavu wa aina tofauti nchini kubaini kuwa asilimia 98% ya makundi ya watoto wenye ulemavu hawaendi shule kwa sababu mbali mbali ikiwemo dhana potofu iliyopo miongoni mwa jamii.  Akizungumza na mamia ya wananchi katika kijiji cha Duga kilichopo kata ya Duga wilayani Mkinga katika zoezi la kuhamisisha jamii kuwapatia haki zao za msingi walemavu  mtaalam wa kuhudumia walemavu kutoka nchini Thailand Dr,Kirsi Salo  amesema katika utafiti wao walioufanya katika mikoa mbali mbali nchini baadhi yao wamefichwa majumbani kutokana na imani haba za kishirikina  kuwa kuzaa mtoto mlemavu ni mikosi ndani ya familia na baadhi ya familia hudiriki hata kupoteza maisha yao. Kwa upande wake kiongozi wa kanisa la kilutheri usharika wa Duga mchungaji Clementi Hongele ambaye amedai ...

SIKU YA MTOTO WA AFRIKA

Image
Siku ya Mtoto wa Afrika na Elimu bora isiyo vikwazo Mtoto akitafakari Juni 16 ya kila mwaka Umoja wa Afrika sambamba na washirika wake husherekea siku ya mtoto wa Afrika- au kwa kimombo Day of African Child (DAC ), ikiwa ni kumbukumbu ya mwaka 1976 ambapo waandamanaji wanafunzi wa shule za Soweto Afrika ya Kusini waliandamana kupinga elimu iliyokuwa inatolewa kwa manufaa ya utawala wa kibaguzi wa makaburu. Maandamano hayo yalipokelewa na mikono usio na huruma na masikio yasiyo sikivu ya utawala wa kibaguzi na kusababisha vifo vya mamia ya wanafunzi “Watu wangu, leo nipo huru nipo huru kwa kuwa sintosahaulika kabisa, siku itatimia ambapo kila mmoja wetu atakuwa huru, huru kutokana na unyanyasaji, huru kutokana na uwoga, huru kutokana na kuuwawa, nyinyi ni vijana wadogo mtaishi hadi kuiona siku hiyo na ata kama sintofanikiwa kuiona siku hiyo nyinyi mnatakiwa kusadiki tu kuwa nitakuwepo siku hiyo, hapa ni nyumbani kwangu, pahala pangu pa kuishi.” Hayo ni ...

AJIRA KWA WATOTO NI ZAO LA UBEPARI.

Image
Tarehe 12 Juni ya  kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ajira kwa Watoto. Katika maadhimisho haya hufanyika makongamano na hafla mbalimbali kujaribu kupiga kampeni dhidi ya ajira za watoto. Tanzania ni miongoni mwa nchi 174 zilizoridhia azimio namba 182 la kukomesha utumikishaji watoto chini ya umri wa miaka 18.  Hakuna anayepinga  juu ya kuwepo ajira za watoto kila mahala. Kwa mfano, kwa mujibu wa uchunguzi wa gazeti la  Mwananchi kupitia mradi wa kupambana na ajira ngumu kwa watoto Zanzibar,  zaidi ya watoto 15,000  ndani ya Zanzibar wanajishughulisha na ajira tena zile ngumu. http://www.mwananchi.co.tz/habari/habari-ya-ndani/Ajira-ngumu--kwa-watoto-Zanzibar/-/1724700/2074082/-/3uj83s/-/index.html Aidha, kuna vilio kama hivyo vya ajira za watoto pia Tanzania  Bara hususan  katika maeneo ya machimbo ya migodini yakiwemo Mererani mkoani Manyara, maarufu kwa uchimbaji wa madini aina tanzanite. http://www.bbc.co.uk...

TAREHE 12/06 KILA MWAKA TUIKUMBUKE SOTE, TUPIGANIE HAKI ZA WATOTO WALIO KATIKA AJIRA MBAYA.

Image
Siku ya kimataifa ya kupinga ajira ya watoto: Ajira na dhuluma za kimapenzi ndio jinamizi kubwa zaidi.   Kila mwaka Juni 12 ni siku ya kimataifa ya kupinga ajira kwa watoto na mwaka huu kauli mbiu ni "funga bao kutokomeza ajira ya watoto". Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF katika kuadhimisha siku hiyo imetoa wito wa hatua za haraka kuchukuliwa kote duniani ili kukata mirija ya ajira mbaya ya watoto. UNICEF pia inasherehekea miaka kumi ya ushirikiano na shirika la IKEA katika kulinda haki za watoto na kupambana na ajira ya watoto. UNICEF inasema dola milioni 190 zilizotolewa kwa ushirikiano zimebadili maisha ya watoto wapatao milioni 100 katika nchi 30 na hivyo kuifanya UNICEF na IKEA kuwa wahisani wakubwa. Wataalamu wawili wa Umoja wa Mataifa kuhusu utumwa na kuuzwa kwa watoto wamesema kuwa zaidi ya watoto milioni 215 wanafanya kazi kote duniani huku zaidi ya nusu yao wakipitia hali ngumu zikiwemo dhuluma za kimapenzi na za kikazi. Aki...

TANZANIA BINGWA KOMBE LA DUNIA KWA WATOTO WA MTANZANIA BINGWA KOMBE LA DUNIA KWA WATOTO WA MITAANI. ITAANI.

Image
FULL TIME!!!! TANZANIA HAVE WON THE STREET CHILD WORLD CUP 3-1 AGAINST BURUNDI!! SO PROUD OF OUR BOYS! TANZANIA BINGWA KOMBE LA DUNIA KWA      WATOTO WA MITAANI. Timu ya taifa ya Tanzania kwa watoto wa mitaa ni imenyakua Kombe la Dunia kwa watoto wa mitaani, katika mashindano yaliyozishirikisha timu za mataifa mbalimbali duniani huko Rio de Janeiro, Brazil hapo jana. Ikiwa imetinga fainali za Kombe la Dunia kwa w TANZANIA BINGWA KOMBE LA DUNIA KWA    WATOTO WA MITAANI. atoto wa mitaani kwa mara ya pili mfululizo, timu hiyo ya Tanzania imeweza kutwaa Kombe la Dunia kwa Watoto wa Mitaani kama linavyojulikana Street Child World Cup hapa Rio de Janeiro. Tanzania imetwaa ubingwa huo baada ya kuonyesha kiwango cha juu hata kuzishinda timu ngumu kama Burundi, Marekani, Indonesia, Nicarague, Ufilipino na Argentina.Katika mechi ya fainali Tanzania iliibanjua Burundi iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa ya kulinyakua kombe hili kwa ...

VIPAJI VILIVYOSAHAULIKA

Image
Tanzania Kucheza Nusu fainali ya Kombe la Dunia la Watoto wa Mitaani, Brazil… By Israel Saria on April 4, 2014 Timu ya Taifa ya Tanzania ya watoto wanaoishi mitaani – Tanzania Street Star kwa mara nyinginge imeweza kufika katika nusu fainali za mashindano ya Kombe la Dunia kwa vijana wanaoishi mitaani ( Street Child World Cup 2014) yanayofanyika kwa mara ya pili toka kuanzishwa na safari hii yakifanyika katika Jiji la Rio de Janeiro. Tanzania leo imeweza kufika fainali baada ya kuifunga moja ya timu ngumu kabisa katika mashindano haya timu ya Indonesia kwenye mechi ya Robo fainali iliyochezwa majira ya asubuhi hapa Rio de Janeiro. Katika mechi hii ya robo fainali Tanzania ilikuwa ya kwanza kupachika magoli ya mapema katika kipindi cha kwanza yakifungwa na Michael pamoja na Hassan. Baada ya magoli hayo Indonesia waliweza kuishambuli Tanzania kwa takribani muda wote wa mchezo wakisaka kurudisha magoli. Indonesia waliweza kusawazisha magoli katika dakika za mwisho z...

ONGEZEKO LA WATOTO WA MITAANI NA OMBAOMBA

Image
IDADI kubwa ya watoto wadogo wanaoishi katika mazingira hatarishi inaweza kutishia amani nchini, ikiwa hatua za makusudi hazitachukuliwa kuokoa kizazi hicho. Hayo yalielezwa jana na Mkurugenzi wa Mradi wa Tuwalee  FHI 360, Levina Kikoyo mara baada ya kufanyika kwa uzinduzi wa ripoti iliyofadhiliwa na Shirika la Misaada na Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID) ya utafiti uliofanyika kuanzia Februari mwaka huu juu ya kasi ya ongezeko la watoto hao. Alisema kwa sasa taifa lina watoto wengi walio katika mazingira hatarishi kutokana na kutopata elimu na kusababisha pia ongezeko la watoto hao mitaani, hali itakayozaa wimbi la ujambazi na uhalifu nchini katika siku za mbele.         Alieleza kuwa kwa sasa zaidi ya watoto milioni 2 wanaishi katika mazingira hatarishi na hata wengine kujihusisha na shughuli za kuomba mitaani, na hivyo kuzua hofu ya matokeo mabaya kwa taifa. Alisema utafiti wao waliofanya katika wilaya zote tatu za Mkoa wa Dar e...