TANZANIA BINGWA KOMBE LA DUNIA KWA WATOTO WA MTANZANIA BINGWA KOMBE LA DUNIA KWA WATOTO WA MITAANI. ITAANI.

FULL TIME!!!! TANZANIA HAVE WON THE STREET CHILD WORLD CUP 3-1
AGAINST BURUNDI!! SO PROUD OF OUR BOYS!

TANZANIA BINGWA KOMBE LA DUNIA KWA     

WATOTO WA MITAANI.

Timu ya taifa ya Tanzania kwa watoto wa mitaani imenyakua Kombe la Dunia kwa watoto wa mitaani, katika mashindano yaliyozishirikisha timu za mataifa mbalimbali duniani huko Rio de Janeiro, Brazil hapo jana.
Ikiwa imetinga fainali za Kombe la Dunia kwa w

TANZANIA BINGWA KOMBE LA DUNIA KWA    WATOTO WA MITAANI.

atoto wa mitaani kwa mara ya pili mfululizo, timu hiyo ya Tanzania imeweza kutwaa Kombe la Dunia kwa Watoto wa Mitaani kama linavyojulikana Street Child World Cup hapa Rio de Janeiro.
Tanzania imetwaa ubingwa huo baada ya kuonyesha kiwango cha juu hata kuzishinda timu ngumu kama Burundi, Marekani, Indonesia, Nicarague, Ufilipino na Argentina.Katika mechi ya fainali Tanzania iliibanjua Burundi iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa ya kulinyakua kombe hili kwa Kuinyuka magoli 3-1 huku mchezaji kiungo mshambuliaji wa Tanzania Frank William akipiga magoli matatu na kuwa nyota wa mchezo. Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Tanzania ilikuwa ikiongoza kwa magoli 2-0. Kipindi cha pili iliongeza bao la tatu. Burundi iliweza kupata bao la kufutia machozi zikiwa zimebakia dakika nne mpira kumalizika.
Golikipa wa Tanzania Emmanuel ameweza kuchaguliwa kuwa golikipa bora wa michuano hii ya kombe la dunia.
Hii ilikuwa mara ya Pili kwa timu ya Tanzania kutinga fainali za michuano hiyo ya dunia kwa watoto wa mitaani inayofanyika siku chache kabla ya fainali za Kombe la Dunia kuanza mwezi Juni. Ikumbukwe kuwa fainali zilizopita za michuano hii kule Durban Afrika Kusini mwaka 2010 Tanzania ilifungwa na India katika fainali.
Mashindano haya hutambuliwa na Shirikisho la Soka Duniani, FIFA.

MATOKEO YA NYUMA.
Timu ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania (TSC) imefanikiwa kutwaa Kombe la dunia mara baada ya kuifunga Timu ya Burundi bao 3-1, ambapo awali kabla ya  kuingia nusu fainali ya mashindano ya Kombe la Dunia yanayofanyika Rio de Janeiro nchini Brazil iliifunga Indonesia kwa jumla ya mabao 5-3.



Hadi muda wa kawaida wa mchezo huo unamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana mabao 2-2 ndipo ikatumia mikwaju ya penalti kuamua mshindi. Tanzania ilipata penalti tatu dhidi ya moja ya wapinzani wao.


Kwa matokeo hayo, Tanzania ikatinga nusu fainali dhidi ya Marekani na kufanikiwa kupata ushindi.

Awali Tanzania ilitoka sare ya mabao 2-2 na Burundi, ikaitandika Argentina mabao 3-0 ikailaza Nicaragua mabao 2-0 na ikafungwa na Philippines mabao 2-0.

HAKUNA BINADAMU ALIYEKO KATIKA HII DUNIA KWA BAHATI MBAYA, KILA MWANADAMU NI MPANGO WA MUNGU...

Leo hii kila kona za nchi ya Tanzania habari ni watoto wa mitaani watwaa kombe la Dunia, tumesahau kama watoto hawa hawa ndio kila siku tunawatukana matusi mazito, tunawapiga vibaya na kuwaumiza, mbaya zaidi wapo wanaobakwa na kulawitiwa huko mitaani, leo hii kila mtu yupo kifua mbele kwa ajili ya hawa watoto, HII imedhihirisha vipawa na vipaji vya pekee Mungu alivyo wajaalia.

Sisemi watu wasijisifu kwa hatua kubwa na ya kipekee waliyoifikia hawa watoto, ila najaribu kuonesha ni kwa namna gani kila mtu ana umuhimu wake hapa Duniani, Tofauti za kimaisha tulizonazo zisiwe sababu za kututenganisha na kudharauliana. 
Hii imetoa picha kamili kuhusu watoto wa mitaani kuwa nao wana umuhimu wao tena mkubwa sana hapa duniani, na hii pia imedhihirisha wazi kuwa watoto hawa achilia mbali mazingira magumu wanayoishi wana vipaji vya kipekee sana, leo imeonekana wazi kwenye mpira la naamini vipo vipaji zaidi ya mpira, kuna waigizaji, wanariadha, mabondia na kila aina ya vipaji tuvijuavyo hapa duniani. 

Kubwa zaidi ili tuweze kuviona vipaji zaidi kutoka katika hili kundi lililosahaurika la watoto wa mitaani ni sisi jamii nzima kwa ujumla wake, Serikali na mashirika binafsi, Taasisi mbalimbali kuguswa na maisha ya hawa watoto tukiamini na wao pia ni watoto kama walivyo watoto wetu majumbani. Tuwasaidie kwa hali na mali ili waweze kuamini na wao pia ni sehemu ya jamii hii tunayoishi.
Huu ni mwanzo mzuri kwa watoto wa mitaani naamini mmewatoa kimasomaso watanzania. 
 wajaalia.

HEAR MY VOICE inatumia fursa hii kusema HONGERENI SANA WATOTO WA MITAANI, Tanzania na Dunia nzima itatambua uwepo wenu na kila kipaji kitaonekana na kuendelezwa.
         MUNGU IBARIKI TANZANIA.... MUNGU WABARIKI WATOTO WA MITAANI.  

Comments

Popular posts from this blog

WATOTO WA MITAANI NA JINSI YA KUWASAIDIA

AYA ZA BIBLIA KUHUSU WATU WENYE ULEMAVU

TUWAKUMBUKE WATOTO WENYE MTINDIO WA UBONGO KAMA KUNDI MAALUM KATIKA JAMII ZETU