HII NI KWA JAMII NZIMA.
Maisha ya hapa dunia ni ya kupita tu, mali na vyote vionekanavyo ni mapito pia . Ila upendo na kuthaminiana bila kujali tofauti zetu ni hazina kubwa sana hapa duniani. Jamii inasikitisha sana yawezekana ni kwa kujua au kutokujua, lakini kweli inasikitisha sana, JANA nimeonekana mtu wa ajabu baada ya kukaa na watoto wa mitaani maeneo ya Bunda stand mpya, Mzee mmoja msomi na mwenye heshima kubwa hapa wilayani alinifuata na kuniambia kwanini nimekaa na watoto wahuni wa mitaani, akaenda mbali zaidi na kusema hawa ndio majambazi wa wilaya hii. Akatokea Dereva mmoja ambaye yeye hata hakutaka kujua nilikuwa naongea nini na wale watoto yeye akawafukuza kwenye viti, mbaya zaidi akawapiga na kuwatupia matusi mazito. Baada ya hapo huyo dereva akaniambia nilikuwa nakuheshimu sana ila leo nimekuchukulia tofauti kabisa, akasema "nilidhani umeenda shule umeelimika kumbe shule haijakusaidia" utakaaje na watoto wachafu namna hii, hawa ni vibaka wa stand wewe unakaa nao. Kweli ilini...