NI WAJIBU WETU.
JAMII IWAJIBIKE KUWASAIDIA WATOTO WA MITAANI, YATIMA.... Kitanda usichokilalia, huwezi kujua kunguni wake, shida na mateso wanayoyapata watoto waishio katika mazingira hatarishi na wale wa mitaani ni vigumu kuyaeleza. Watoto hawa hawajui leo au kesho watakula nini, hakuna anayehangaika kuwatafutia chakula, wanapolala na njaa hakuna wa kumlilia na wakiumwa hakuna wa kumweleza hivyo huendelea na maisha yao hadi wanapopata nafuu au kupona kabisa. Ukweli ni kwamba, watoto hawa hujisikia wapweke kutokana na jamii kubwa kuwakataa na kuwaweka katika fungu tofauti. Jambo la kusikitisha ni idadi kubwa ya watoto hawa umri wao unaanzia miaka miwili hadi kumi ambao kimsingi hawajui kujitegemea, njaa ikiuma wanalia tu na kushindwa kujieleza. Kitanda chao ni barabarani na wengine mitaroni, baridi yote ya usiku na jua la mchana ni lao ,hawajui kubadilisha nguo, zile walizovaa wiki iliyopita hadi leo hazijatoka mwilini, Tumezo...