Posts

Image
  FULL NAME;  SANJI   JAMES  MIRUMBE EDUCATION; Bachelor of education in special needs PROFESSIONAL; Specialist teacher and Mental Health Specialist  Why I decide to create this blog. First of all I thank God for who I am, I thank Him for his love and for this case I think it is my time now to return to God what He gave me. What I always walk with, is divine law of God that is law of love, that “you shall love God at the same time love others” and another is golden law that “do to others things that you want them to do to you. Why am I saying this? You see these days there is a lot of suffering and miseries many inhuman practice to vulnerable children, they are helpless and they need someone to her their voice, why should I think of them? It is because God did it to me at a first time, so now it is my time to return the favor. JOHN: 13:15:1  have set you an example that you should do as I have done for you. From this fact I made this blog for the vulnerable children to be the voice of

TAARIFA KWA UMMA

                 HEAR MY VOICE INARUDI KAZINI KUANZIA TAR 01/04/2022. NAPENDA KUWATAARIFU WASOMAJI WA HEAR MY VOICE BLOG, BAADA YA KUTOKUWA HEWANI KWA MUDA KUTOKANA NA MATATIZO YA KIMFUMO, SASA UTAANZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU KWA HARAKA NA USAHIHI.  1. WATOTO WENYE ULEMAVU 2. WATOTO WA MITAANI. IMETOLEWA NA  SANJI JAMES MIRUMBE  MWANZILISHI WA HEAR MY VOICE.  13/03/2022

TULITAFAKARI HILI

Image
Ni Watoto wa Mitaani sawa, lakini Vipaji vyao vyaweza kuleta Manufaa au Kuangamiza Taifa hili (1500) Views Ukipita katika viunga vya miji mikubwa ya Tanzania, kuanzia Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma, Morogoro na kadhalika, hushangai kukuta watoto wakizurura mitaani huku wakati wa usiku wakiwa wamejilaza katika vibaraza vya maduka na katika maeneo ya wazi kama kwenye viwanja vya michezo. Kwao mvua ni yao, baridi ni yao na jua pia ni lao. Watoto hao wanaishi katika mazingira hatarishi yanayowaweka katika vishawishi vya kufanya uhalifu, kama vile uporaji na kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na biashara nyigine yoyote ile haramu.  Katika hali ya kukosa chakula, malazi na mavazi kama mahitaji muhimu ya mwanadamu, watoto hawa wamekuwa wakisukumwa kujihusisha na vitendo vya kihalifu kama njia ya kujipatia riziki. Wanapokuwa katika mazingira hayo, wanaweza kuja kuwa watu hatari na tishio kwa taifa hili, hivyo kuigeukia jami

HILI NI LA KUANGALIA KWA JICHO LA PEKEE....

Image
Tanzania ina shule moja tu ya sekondari ya viziwi! Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Elimu Maalumu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufindi Estrida Kimweri akieleza changamoto ya kuwa na shule moja ya sekondari kwa walemavu viziwi. Tanzania inakabiliwa na changamoto ya kuwa na shule moja ya sekondari kwa walemavu wasiosikia, toka ipate uhuru, hii haiendani na sheria ya mwaka 2010 ya walemavu ambayo inatetea kundi hilo kupata elimu. Akizungumza katika mahojiano maalum na Taarifanews.com Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Elimu Maalumu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Estrida Kimweri, changamoto hiyo inapelekea kukosa idadi kubwa ya walemavu wa aina hiyo wanaomaliza mpaka shule ya sekondari. Kimweri alisema kuwa shule hiyo ipo mkoa wa Njombe na kuna wanafunzi wengi sana wanaoletwa kutoka katika shule mbalimbali, kupata elimu ya sekondari kwenye shule hiyo, lakini nafasi yake ni ndogo sana kuweza kupokea wanafunzi wengi. Kwa sas

MFANO WA KUIGWA NA WENGINE WENYE NAFASI YA KUISAIDIA HII JAMII,, NI JUKUMU LETU SOTE.

Image
GOLA KUWAONDOA WATOTO WA MITAANI JIJINI ARUSHA Afisa ustawi wa jamii na Maendeleo ya jamii jijini Arusha Mwantumu Dossi akitembelea mradi wa shamba la mahindi unaoendeshwa na taasisi ya Gola Foundation jana katika kituo cha Kufikia watoto wa mitaani,katikati ni Mkurugenzi wa shirika hilo Elisha Maghembe habari picha na l ibeneke la kaskazini blog Mkurugenzi wa shirika lisilokua la kiserikali la Gola Foundation Elisha Maghembe amesema kuwa wameanza zoezi la kuwaondoa watoto wa mitaani walioko jijini Arusha na kuwafikisha kwenye vituo maalumu vya malezi lengo ikiwa ni kuwarudisha makwao pamoja na kuwapatia fursa ya elimu waliyoikosa kwa muda mrefu. Elisha alisema kuwa zoezi hilo limeanza mapema mwaka huu ambapo mpaka sasa wamewakusanya watoto 25 na kuwapeleka katika kituo chao cha malezi kilichopo wilaya ya Arumeru ambapo watoto watano walitambuliwa na kuchukuliwa na wazazi wao. Amesema kuwa watoto wa mitaani wanapokaa mtaani kwa muda mrefu hujitumbukiza

NI JUKUMU LETU SOTE KUFANIKISHA ELIMU JUMUISHI

MWANZONI mwa mwaka 2009,  mke wa Rais,  Salma Kikwete aliitaka jamii kutowatenga wanafunzi wenye ulemavu badala yake wasaidiwe  na kushirikishwa  katika masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo kupewa elimu kama ilivyo kwa makundi mengine ya kijamii. Siku aliyotoa wito huo hakusita kusema kuwa zaidi ya Sh milioni 881 zinahitajika kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kusomea kwa wanafuzi 8700 wenye ulemavu nchini ili waweze kujifunza katika hali mazingira mazuri. Tunapozungumzia mazingira mazuri kwa wanafunzi wenye ulemavu hatumaanishi vifaa na mahitaji mengine ya kitaaluma pekee  bali hata miundombinu kama vyumba vya madarasa, vyoo, maktaba, maabara, mabweni na mazingira ya eneo zima la shule Kufanya hivi ni kuwapa fursa ya wao kujiona kuwa ni sehemu ya jamii hali itakayowapa ari ya kujifunza sambamba na wenzao wasiokuwa na ulemavu. Hili ni wazo zuri sana na naaunga na wewe Mama Salma KIkwete ila wazo hili mpaka kufikia leo 2015 halijafanikiwa kwa kiasi kikubwa hii ikiwa inasabab

TAFAKARI,,,, CHUKUA HATUA.

Image
Jamii inapaswa kutambua na kuweka mazingira sahihi kwa ajili ya Walemavu (835) Views ULEMAVU ni athari ya muda mfupi au ya kudumu inayosababishwa na hitilafu za kiwiliwili au hisia mfano uoni, usikivu, akili, kusema na kumsababishia mtu kushindwa kufanya kazi kikawaida. Jamii ya watu wenye ulemavu nchini ni kundi kubwa miongoni mwa takribani ya watanzania milioni 45, ambao wamesahaulika katika sekta mbalimbali kutokana na jamii kuwatenga na kusahaulika kabisa bila kuwasaidia katika maisha ya kila siku. Kwa miaka mingi, suala la ulemavu halikupewa umuhimu na uzito wowote katika jamii kutokana na mitizamo na imani potofu.  Kuna aina nyingi za ulemavu, kuna ulemavu wa viungo, ulemavu wa uoni, kiziwi na matatizo ya kusema, ulemavu wa akili, albino (ulemavu wa ngozi) mwingineo kama kifafa, kichwa kikubwa mpasuko wa mdomo pamoja na ulemavu mchanganyiko ambapo mtu anakuwa na ulemavu zaidi ya mmoja katika jamii tunayoishi. Wahenga walinena kuwa “hujafa hujaumbika” na “usimtukane