NI JUKUMU LETU SOTE KUFANIKISHA ELIMU JUMUISHI

MWANZONI mwa mwaka 2009,  mke wa Rais,  Salma Kikwete aliitaka jamii kutowatenga wanafunzi wenye ulemavu badala yake wasaidiwe  na kushirikishwa  katika masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo kupewa elimu kama ilivyo kwa makundi mengine ya kijamii.
Siku aliyotoa wito huo hakusita kusema kuwa zaidi ya Sh milioni 881 zinahitajika kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kusomea kwa wanafuzi 8700 wenye ulemavu nchini ili waweze kujifunza katika hali mazingira mazuri.
Tunapozungumzia mazingira mazuri kwa wanafunzi wenye ulemavu hatumaanishi vifaa na mahitaji mengine ya kitaaluma pekee  bali hata miundombinu kama vyumba vya madarasa, vyoo, maktaba, maabara, mabweni na mazingira ya eneo zima la shule
Kufanya hivi ni kuwapa fursa ya wao kujiona kuwa ni sehemu ya jamii hali itakayowapa ari ya kujifunza sambamba na wenzao wasiokuwa na ulemavu.
Hili ni wazo zuri sana na naaunga na wewe Mama Salma KIkwete ila wazo hili mpaka kufikia leo 2015 halijafanikiwa kwa kiasi kikubwa hii ikiwa inasababishwa na changamoto zifuatazo;
  • uhaba wa waalimu wenye taaluma ya elimu maalumu
  • mitazamo hasi ya jamii kuhusu walemavu
  • mitazamo hasi ya wazazi juu ya watoto wao walemavu
  • mitazamo hasi ya walimu wasio na taaluma ya elimu maalumu
  • mitazamo hasi ya wanafunzi wasio na ulemavu
  • ubadhirifu wa viongozi katika idara ya elimu maalumu
  • jamii kuwatumia walemavu kama mtaji
hizi ni baadhi ya sababu zinazokwamisha walemavu kupata elimu sawa na wasio na ulemavu japo serikali na baadhi ya wadau wamekuwa wakipigia kelele suala la elimu jumuishi lakini kwa sababu tajwa hapo juu imekuwa ni ndoto katika kulifanikisha wazo hilo. 
nitazungumza kwa mapana sababu moja baada ya nyingine kwa kina na mifano makini

Leo naanza na:

  • Mitazamo hasi ya walimu wasio na taaluma ya elimu maalumu.
Mwalimu kama mdau muhimu katika elimu ni mategemeo ya kila mmoja mwalimu awe ni kiungo muhimu katika kufanisha suala la elimu jumuishi, lakini kwa bahati mbaya kuna baadhi ya walimu wenye shahada na stashahada za ualimu kutoka katika vyuo vinavyotambulika na serikali wamekuwa ni kikwazo kikubwa kwa kufanikisha elimu jumuishi kwa baadhi ya shule, hii inatokana na mitazamo hasi waliyonayo kuhusu ulemavu na watoto wenye ulemavu katika shule zao, hii inaanzia kwa wakuu wa shule hizo na walimu wao, mfano nilkiwa mwaka pili chuo nilifanya field katika moja ya shule jumishi jijini mwanza, siku ya kulipoti kituoni mkuu wa shule alifurahi sana kuwa amepata walimu ila katika kujitambulisha yule mkuu wa shule akakili amepta mzigo kwa kumaanisha walimu wa elimu maalumu anaona hawana kazi, bahati mbaya alienda mbali zaidi kwa kusema yeye hawezi kumshauri mwanae asome elimu maalumu ni kupoteza muda. huyo ni mkuu wa shule mtu aliye na dhamana ya kuhakikisha watoto wenye na wasio na ulemavu wanapata elimu sawa anakuwa na mtizamo wa namna hiyo itakuwaje kwa walimu mwake wasio na taaluma ya elimu maalumu?

lakini mfano huu unazikumba shule nyingi tu kwa kuwaona watoto wenye ulemavu kama ni watoto wasiostahili kupata elimu sawa na wasio na ulemavu. Hii inatokana na kuwajengea mazingira magumu hasa katika kuwafundisha na baadhi ya majina wanayowapachika kama vile, kilaza na mengine mengi. Hii inawavunja moyo wanafunzi na wengi wao wanaacha shule kwa kuamini hawana uwezo wa kusoma sawa na wenzao. 

 Ushauri wangu, walimu wasio na taaluma ya elimu maalum saidieni juhudi za serikal na wadau wengine kwa kuwachukulia wanafunzi wote sawa, zaidi kuwatia moyo wenye ulemavu ili nao wajione ni sehemu ya jamii inayowazanguka. 

Comments

Popular posts from this blog

WATOTO WA MITAANI NA JINSI YA KUWASAIDIA

AYA ZA BIBLIA KUHUSU WATU WENYE ULEMAVU

TUWAKUMBUKE WATOTO WENYE MTINDIO WA UBONGO KAMA KUNDI MAALUM KATIKA JAMII ZETU