MFANO WA KUIGWA NA WENGINE WENYE NAFASI YA KUISAIDIA HII JAMII,, NI JUKUMU LETU SOTE.
GOLA KUWAONDOA WATOTO WA MITAANI JIJINI ARUSHA
Afisa ustawi wa jamii na Maendeleo ya jamii jijini Arusha Mwantumu Dossi akitembelea mradi wa shamba la mahindi unaoendeshwa na taasisi ya Gola Foundation jana katika kituo cha Kufikia watoto wa mitaani,katikati ni Mkurugenzi wa shirika hilo Elisha Maghembe
habari picha na libeneke la kaskazini blog
Mkurugenzi wa shirika lisilokua la kiserikali la Gola Foundation Elisha
Maghembe amesema kuwa wameanza zoezi la kuwaondoa watoto wa mitaani
walioko jijini Arusha na kuwafikisha kwenye vituo maalumu vya malezi
lengo ikiwa ni kuwarudisha makwao pamoja na kuwapatia fursa ya elimu
waliyoikosa kwa muda mrefu.
Elisha alisema kuwa zoezi hilo limeanza mapema mwaka huu ambapo mpaka
sasa wamewakusanya watoto 25 na kuwapeleka katika kituo chao cha malezi
kilichopo wilaya ya Arumeru ambapo watoto watano walitambuliwa na
kuchukuliwa na wazazi wao.
Amesema kuwa watoto wa mitaani wanapokaa mtaani kwa muda mrefu
hujitumbukiza katika majanga ya matumizi ya madawa ya kulevya na kufanya
vitendo visivyofaa hivyo ameitaka jamii ishirikiane kutatua tatizo hili
ambalo ni janga kwa taifa.
“Tunapofika mtaani kuwaondoa watoto hawa wa mtaani tunakutana na
changamoto nyingi ikiwemo kukosa ushirikiano na watoto wenyewe na pia
wengine wanatumkishwa na ajira katika umri mdogo na baadhi ya watu hivyo
kufanya zoezi hilo kuwa gumu” Alisha Elisha
Afisa ustawi wa jamii na Maendeleo ya jamii jijini A Mwantumu Dossi
alifika katika kituo cha kufikia cha malezi ya watoto wa mtaani
kinachomilikiwa na Gola Foundation amesema kuwa Halmashauri ya jiji
itaangalia namna ya kushirikiana kutatua changamoto za watoto wa
mitaani.
“Tatizo la watoto wa mitaani ni tatizo sugu nimefika apa kujionea na
kama Jiji kuna mkakati Mahususi wa kuwaondoa watoto wa mitaani
utakaoanza 2015-2016” alisema Mwantumu
Mwenyekiti wa Baraza la watoto wilaya ya Arusha
Hassan Omari alisema kuwa juhudi za kuwaondoa watoto wa mitaani katika
mazingira magumu na hatarishi zinapaswa kuungwa mkono na kila mtu pamoja
na serikali kwani watoto ni taifa linalotegemewa kesho.
Comments
Post a Comment