HILI NI LA KUANGALIA KWA JICHO LA PEKEE....
Tanzania ina shule moja tu ya sekondari ya viziwi!
Akizungumza katika mahojiano maalum na Taarifanews.com Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Elimu Maalumu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Estrida Kimweri, changamoto hiyo inapelekea kukosa idadi kubwa ya walemavu wa aina hiyo wanaomaliza mpaka shule ya sekondari.
Kimweri alisema kuwa shule hiyo ipo mkoa wa Njombe na kuna wanafunzi wengi sana wanaoletwa kutoka katika shule mbalimbali, kupata elimu ya sekondari kwenye shule hiyo, lakini nafasi yake ni ndogo sana kuweza kupokea wanafunzi wengi.
Kwa sasa hapa nchini kuna walemavu wapato milioni 6 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012, lakini pia kuna aina mbalimbali kama walemavu wasioona, walemavu wa viziwi wasiona, walemavu wa ngozi, walemavu wa viungo na walemavu wa akili.
Comments
Post a Comment