SIKUKUU KWA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU KWAO NI SIKU YA MATESO.
                     Baadhi ya watoto wa mitaani wakiwa wamelala nje kutokana na kukosa  sehemu za kulala.Baadhi yao kwa kutaka sehemu nzuri za kulala na chakula  kizuri huwa tayari kufanyiwa vitendo vibaya.          Watoto kulawitiwa ili wapate hifadhi ya kulala  au kupewa chakula kizuri ni sehemu ya maisha ya baadhi ya watoto waishio  mitaani mjini. Hii ni siri kubwa ambayo imejificha miongoni mwao,  ili uweze kupata siri hii inakulazimu lazima ujenge uhusiano wa karibu  na wa muda mrefu na watoto hao.       Watuhumiwa wakubwa wa kuwaingilia kinyume na  maumbile watoto hao ni baadhi ya walinzi wanaolinda katika maduka ya  biashara na vijana waliowazidi umri; vitendo hivyo vinaonekana  kushika  kasi.      Uchunguzi wa kina uliofanywa na Mwandishi wa  makala haya kwa miezi kadhaa, umebaini kuwa vitendo vichafu  vimesababisha baadhi yao kuathirika kisaikolojia hivyo kujikuta wakiona  jambo hilo ni la kawaida na hulifurahia.      Watoto hao hufanyiwa vitendo hivyo hasa kipindi  ...