MTOTO ANITHA ANAHITAJI KUSAIDIWA
Mtoto ANITHA
Masikini mtoto mlemavu Anitha
Mtoto Anitha akiinua kichwa kwa
shida. Picha na Lilian Lugakingira .
Kagera. “Jinsi nilivyoangaika na mtoto huyu najisikia kukata tamaa
ila sina jinsi, naomba tu Mungu anisaidie aniongezee moyo wa uvumilivu na
subira hadi atakapopona,” hii ni kauli ya Juster Vedasto (26) mkazi wa eneo la
Kamizilente Kata ya Rwamishenye katika manispaa ya Bukoba, ambaye mtoto wake
amevimba kichwa kwa zaidi ya miaka mitatu sasa kutokana na kujaa maji.
Mtoto huyo Anitha Alex mwenye umri wa
miaka mitatu na miezi kumi na mmoja alipatwa na tatizo hilo la kuvimba kichwa
akiwa na umri wa miezi mitatu, kwa mujibu wa mama yake, alianza kuvimba sehemu
za utosini na baadae kichwa kizima.
Mtoto huyo ambaye mwaka jana kupitia
vyombo vya habari aliomba kupatiwa msaada kwa ajili ya kwenda Hospitali ya KCMC
mkoani Kilimanjaro kupatiwa matibabu ya kichwa, bado anahitaji kusaidiwa ili
aendelee na matibabu.
Kwa mujibu wa mama yake, msaada
aliopatiwa mwaka jana ulimwezesha kwenda katika hospitali hiyo na kufanyiwa
upasuaji wa kichwa Juni 5, 2012 aliwekewa mpira kwa ajili ya kutoa maji
kichwani.
Juster anasema mtoto wake alitakiwa
kurudishwa katika hospitali hiyo Februari 15 mwaka huu kwa ajili ya
kubadilishiwa mpira aliowekewa kichwani, lakini hana hata nauli, achilia mbali
gharama za matibabu.
“Nilipofika Moshi mwaka jana
nilipata msamaria mwema aitwaye Benedicto Tarimo ambaye alinipa makazi na
huduma zote muhimu na sasa nikipata nauli nategemea niende kumwomba tena msaada
kama alionipa mwaka jana, kwa sasa sina mawasiliano naye baada ya simu yangu
kuibiwa” anasema Juster.
Mtoto huyo ambaye anakaribia umri wa
miaka minne sasa bado hajaweza kusimama wala kutembea ambapo pia Februari 18
mwaka huu alitakiwa kupelekwa katika kitengo cha mazoezi kilichoko katika hospitali
hiyo ili aanze kufanyishwa mazoezi ya kusimama.
“Tangu alipofanyiwa upasuaji wa
kwanza naona kuna mabadiliko, sasa naona shingo imekaza ilikuwa inalegea,
ameanza kukaa mwenyewe wakati kabla ya upasuaji alikuwa analala muda wote
asingeweza kukaa, nina imani atapona naomba Watanzania wasinichoke.
Juster anasema hana uwezo wa
kufungua akaunti katika benki na kuwa akiifungua hana uwezo wa kupata fedha za
kuweka hivyo anawaomba wanaohitaji kumsaidia watumie namba yake ya simu ambayo
ni 0765230488 hata kwa kumtumia ujumbe mfupi wa maandishi.
pole sana mama Anitha mungu ni mwema utamponya mtoto wako.
ReplyDelete