NI JUKUMU LANGU MIMI, WEWE NA YULE......



USHAURI WANGU KWA JAMII.
JAMII inatakiwa kuwa na upendo pamoja na huruma kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwasaidia, kuepuka changamoto zinazowakabili. Ipo haja ya jamii kubadili mtazamo ilionao dhidi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu na mitaani na kuwapa misaada mbalimbali, ili wajione sehemu ya watoto wengine wanaoishi na kulelewa na wazazi wao ili watoto hawa wawe na maisha mazuri na kupata elimu kama ilivyo kwa watoto wanaolelewa na wazazi pamoja na familia zao, ni vyema jamii ikawa na mwamko wa kutambua changamoto zinazowakabili.
Serikali peke yake haiwezi kuubeba mzigo huu pasipo msaada wa wananchi, takwimu zilizopo zinaonesha zaidi ya asilimia 52 ya watoto wanaishi katika mazingira magumu na mitaani, hivyo ili kuondoa tatizo hili, ni vyema kila mwananchi akawa na huruma itakayomfanya ajipe jukumu la kuwasaidia  watoto hawa, endapo kila mwananchi atajitokeza na kutoa huduma japo kwa mtoto mmoja anayelelewa katika kituo, ama kumchukua na kwenda kuishi naye nyumbani kwake, itakuwa msaada mkubwa kwa Serikali na hivyo kuipunguzia jukumu zito ililonalo.
Pia mashirika binafsi ni vema yakawa ni sehemu ya kupunguza tatizo kwa kutoa vipaumbele katika kuwasaidia hawa watoto kwa kuanzisha vituo vitakavyoweza kuwalea hawa watoto, na makampuni mbalilmbali yaguswe kwa namna moja au nyingine katika kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu na mitaani.
NI JUKUMU LANGU, NI JUKUMU LAKO, NI JUKUMU LETU SOTE KUWAPENDA NA KUWASAIDIA WATOTO HAWA WAISHIO KWENYE MAZINGIRA MAGUMU NA MITAANI.
IMEANDIKWA NA:
SANJI MIRUMBE JAMES. MWANZILISHI NA MMILIKI WA HEAR MY VOICE BLOG.

Comments

  1. ni kweli ni jukumu letu.

    ReplyDelete
  2. Hili ni tatizo kubwa sana ktk Nchi zinazoendelea ikiwemo Tz,maisha ya watu ni magumu,omba omba ni wengi,bomu la watoto wa Mitaani ni kubwa hasa Mijini,.Hii inaonesha ni kwa jinsi gani cc kama wasomi tulivyo na changamoto ya kutoa elimu kwa lengo la kupunguza tatizo hili,nakupongeza sana kaka kwa hili unalolifanya,most of Tz leaders hawaguswi na matatizo ya masikini coz hawategemei kupata kitu kwao while hutegemea kuwasaidia matajiri kwa kutegemea kusaidiwa kwa namna mbalimbali ktk vipindi flan flan.Tz ya leo ni ya wachache wenye nazo na wengi maskini wa kutupwaaaa na kuomba ndiyo ajira pekee rahc kwao,km watoto wako ktk msingi huo je Taifa hl baada ya miaka 30 litatawalika kweli?,tusiache kusema pale inapobidi kwani mimi naamini hatuwezi kutatua matatizo kwa level moja ya kufikiri,lazima kuwe na mawazo kinzani ili kuleta ufanisi.MUNGU BARIKI TAIFA HILI,MUNGU BARIKI KIZAZI HIKI...

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

WATOTO WA MITAANI NA JINSI YA KUWASAIDIA

TUWAKUMBUKE WATOTO WENYE MTINDIO WA UBONGO KAMA KUNDI MAALUM KATIKA JAMII ZETU

AYA ZA BIBLIA KUHUSU WATU WENYE ULEMAVU