YOTE YANAWEZEKANA CHINI YA JUA.
MUNGU ANABADILI MAISHA. RACHEL MWANZA, KUTOKA MTOTO WA MITAANI HADI MCHEZA FILAMU NYOTA AFRIKA. KINSHASA, DRC MAISHA ya mwigizaji Rachel Mwanza yamebadilika katika miaka ya hivi karibuni. Binti huyo mdogo alikuwa mmoja wa watoto waliozagaa mitaani katika Jiji la Kinshasa nchini DRC, lakini hivi sasa ni mmoja wa wacheza filamu nyota barani Afrika. Mbali na kuwa mwigizaji nyota, Rachel ameshinda tuzo nyingi na pia kutembelea katika miji mbalimbali mikubwa duniani kwa ajili ya kupokea tuzo. Binti huyo alikuwa akikatiza katika moja ya mitaa ya Kinshasa wakati nafasi ya kuigiza filamu ya Rabelle (War Witch) ilipomshukia. Waandaaji wa filamu hiyo walibahatika kumuona katika kipindi kimoja cha televisheni cha watoto wa mitaani kilichorushwa nchini DRC na kuvutiwa naye. Ilikuwa ngeke...