NGUVU KAZI INAYOPOTEA
HAYA NDIYO MALAZI YA HUYU MTOTO
WATOTO HAWA HAWANA KAZI MAALUMU
IWE MCHANA AU USIKU SEHEMU YA KULALA KWAO NI TATIZO.
Tatizo la watoto wa mitaani na vijana wa mitaani
limekuwa ni tatizo sugu na linalozidi kuongezeka siku hadi siku. Watoto hawa
wanaishi mazingira hatarishi na wanazikosa haki zao za msingi kama vile elimu,
malezi bora na mahitaji muhimu kama chakula mavazi na malazi
Watoto hawa ndio wanakuwa vijana wa mitaani
wanapokuwa wakubwa, kundi hili la vijana wa mitaani limekuwa ni kundi kubwa na
lisilo na kazi yoyote ya kufanya mitaani hali inayotoa nafasi kwa vijana hawa kujihusisha
na makundi hatari ya uvutaji na utumiaji wa madawa ya kulevya na kusababisha
nguvu kazi ya jamii na taifa kwa ujumla kupotea, vijana wenyewe kushindwa kuwa
na mwelekeo na mtazamo chanya dhidi ya maisha yao ya sasa na baadaye
Hali hii ya uwepo wa watoto wa mitaani
inasababishwa na sababu nyingi zikiwemo umasikini, utengano wa familia na vifo
vinavyosababishwa na ugonjwa hatari wa UKIMWI.
Comments
Post a Comment