AJIRA KWA WATOTO NCHINI TANZANIA BADO NI TATIZO SUGU

Watoto hawa niliowakuta katika Kijiji cha Mlanzi Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani, wakiwa wamebeba ndoo na madumu ya maji kwenye baiskeli, kazi hiyo ya kubeba maji kwa kutumia baiskeli wanalipwa kwa ndoo moja Tsh. 200.
"Shule imefunguliwa tarehe 14 January lakaini mpaka sasa sijaenda kwa sababu ya sina sare ya shule, viatu na madaftari mama ajaninunulia, nafanya kazi ya kuwachotea wanakijiji maji kwa ndoo Tshs. 200 mpaka nipate pesa ya kutosha kununua yunifomu za shule, viatu na madaftari," walisema watoto hao. Bei ya sare za shule kwa sasa ni kuanzi Tshs. 10,000 hadi Tshs.13,000, daftari linauzwa kuanzi Tshs. 500 hadi Tshs 3000.
Kwa siku amepata pesa nyingi ni Tshs. 2000 atauza maji mpaka lini ili apate pesa ya kununua vifaa vya shule? Mzazi wajibu wake ni upi kwa mtoto kama huyu? kuwa na aina hii ya wazazi je utumikishwaji wa watoto utaisha hapa nchini? Kijiji cha Mlanzi kinauhaba wa maji safi na salama, wakazi wengi hasa wanawake hutumia muda mwingi kusubiri maji kisimani.

Shared  on Mkumbaru Blog

Comments

Popular posts from this blog

WATOTO WA MITAANI NA JINSI YA KUWASAIDIA

AYA ZA BIBLIA KUHUSU WATU WENYE ULEMAVU

TUWAKUMBUKE WATOTO WENYE MTINDIO WA UBONGO KAMA KUNDI MAALUM KATIKA JAMII ZETU