USHAURI WANGU KWA JAMII. JAMII inatakiwa kuwa na upendo pamoja na huruma kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwasaidia, kuepuka changamoto zinazowakabili. Ipo haja ya jamii kubadili mtazamo ilionao dhidi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu na mitaani na kuwapa misaada mbalimbali, ili wajione sehemu ya watoto wengine wanaoishi na kulelewa na wazazi wao ili watoto hawa wawe na maisha mazuri na kupata elimu kama ilivyo kwa watoto wanaolelewa na wazazi pamoja na familia zao, ni vyema jamii ikawa na mwamko wa kutambua changamoto zinazowakabili. Serikali peke yake haiwezi kuubeba mzigo huu pasipo msaada wa wananchi, takwimu zilizopo zinaonesha zaidi ya asilimia 52 ya watoto wanaishi katika mazingira magumu na mitaani, hivyo ili kuondoa tatizo hili, ni vyema kila mwananchi akawa na huruma itakayomfanya ajipe jukumu la kuwasaidia watoto hawa, endapo kila mwananchi atajitokeza na kutoa huduma japo kwa mtoto mmoja anayelelewa katika kituo, ama kumch...