Posts

Showing posts from May, 2013

TANZANIA IMECHUKUA HATUA KUKOMESHA AJIRA KWA WATOTO IFIKAPO MWAKA 2015.

TANZANIA YASHUGHULIKIA KUKOMESHA AJIRA KWA WATOTO Kutokana na Utafiti wa Kazi ngumu na Ajira kwa Watoto wa mwaka 2005-2006, karibia asilimia 18 ya watoto wa kati ya umri wa miaka 5 na 17 wanafanya kazi katika mazingira hatarishi kama vile kilimo cha biashara, ukahaba, madini, kazi za nyumbani na uvuvi. "Ajira kwa watoto bado ni tatizo nchini, lakini kupitia jitihada za pamoja serikali inatarajia kukomesha ifikapo mwaka 2015,"   Ni kauli nzuri sana kama itakuwa katika vitendo, ila suala hili si la kuiachia serikali peke yake. Sisi kama tuna jukumu zito sana katika kuhakikisha watoto wote wanaishi maisha yenye usawa na kuacha kuwatumikisha watoto katika kazi ambazo hata kama wao ni masikini kiasi gani sio vizuri kuwatumikisha kama wanyama. Suala la misingi hapa ni watu wote katika jamii tuwe na hofu ya Mungu na vilevile tujiulize maswali, kwa mfano hao watoto tunaowatumikisha kwa kazi ngumu je ndio wangekuwa ni watoto wetu wanatumikishwa hivyo tungejisikiaje? Tuamini

WITO KWA WAZAZI

OFISA ELIMU ATAKA WAZAZI WASIWAFICHE WATOTO WALEMAVU OFISA Elimu wa Manispaa ya Iringa anayeshughulikia elimu ya msingi, Angelous Kisiga, amewataka maofisa watendaji wa kata, mitaa na wenyeviti wa vitongoji katika manispaa hiyo, kuendesha msako wa kuwafichua wazazi wenye tabia ya kuwaficha watoto wenye ulemavu ili wasipatiwe elimu. Akizungumza na MTANZANIA jana, ofisa elimu huyo alisema kuna baadhi ya wazazi wenye tabia ya kuwaficha watoto wenye ulemavu badala ya kuwapeleka shuleni, jambo ambalo ni sawa na ubaguzi. Aliwataka kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kuanza masomo wanapelekwa shule bila kujali kama ni walemavu au siyo walemavu. Pia aliwataka wakazi wa manispaa hiyo, kusaidiana na Serikali katika kuwafichua wazazi wenye tabia hiyo ya kuwaficha watoto wenye ulemavu, ili wapatiwe elimu kama ilivyo kwa watoto wasiokuwa walemavu. Kisiga alisema watoto wote bila kujali ulemavu wao, wanayo haki ya msingi ya kupatiwa elimu, jam

HALI MBAYA

Image
WATOTO WA MITAANI WAGUNDUA AJIRA KATIKA MIJI MBALIMBALI, WASAFISHA VIOO VYA MAGARI NA KUOMBA PESA KWA KAZI HIYO MTOTO AMBAE JINA LAKE HALIKUPATIKANA AKIOSHA KIOO CHA GARI LILILOKUWA LIKISUBIRI KURUHUSIWA KUPITA KATIKA MATAA YA MIANZINI. WATOTO HAO HUSAFISHA VIOO NA KUOMBA PESA KWA MADEREVA HAPA KIJANA ALIYEKUWA AKIOSHA GARI AKIONEKANA AKIOMBA UJIRA WAKE BAADA YA KUMALIZA YA KUSAFISHA KIOO, HATA HIVYO HULAZIMISHA KUFANYA SHUGHULI HIYO BILA MAKUBALIANO YOYOTE.

SIMULIZI YA KWELI

Nililazimika kulala kwenye mitaro ili niweze kuiona kesho Miaka takribani saba iliyopita kwenye mtaa fulani hapa Njombe katika usiku wa giza zito uliofunikwa na baridi kali iliyochangamana na ukungu, wapo vijana kadhaa wamelala chini ya mitaro, wamesogeleana karibu ili angalau wapate joto katika miili yao. Mashuka yao ni maboksi yaliyotolewa vitu vya thamani na kutupwa jalalani. Kati ya vijana hawa ambao wamelala chini ya moja ya mitaro ya mji huu wa Njombe yupo kijana aitwaye John Mwingira ambaye kabla ya miaka saba iliyopita alikuwa akiishi nyumbani kwao Ifakara, wilayani Kilombero mkoani Morogoro. Huko alikuwa akiishi na wazazi wake wote wawili, lakini baadaye wazazi wake waliachana kufuatia kutokuwepo maelewano baina yao. Baba yake akahamia Njombe na mama yake akabakia Ifakara. “Baada ya wazazi wangu kuachana maisha yalikuwa magumu pale nyumbani Ifakara hivyo mama akanishauri nimfuate baba hapa Njombe, nilifika Njombe na kuonana na baba yangu am