TANZANIA IMECHUKUA HATUA KUKOMESHA AJIRA KWA WATOTO IFIKAPO MWAKA 2015.
TANZANIA
YASHUGHULIKIA KUKOMESHA AJIRA KWA WATOTO
Kutokana na Utafiti wa Kazi ngumu na Ajira kwa
Watoto wa mwaka 2005-2006, karibia asilimia 18 ya watoto wa kati ya umri wa
miaka 5 na 17 wanafanya kazi katika mazingira hatarishi kama vile kilimo cha
biashara, ukahaba, madini, kazi za nyumbani na uvuvi.
"Ajira kwa watoto bado ni tatizo nchini,
lakini kupitia jitihada za pamoja serikali inatarajia kukomesha ifikapo mwaka
2015,"
Ni kauli nzuri sana kama itakuwa katika vitendo,
ila suala hili si la kuiachia serikali peke yake. Sisi kama tuna jukumu zito
sana katika kuhakikisha watoto wote wanaishi maisha yenye usawa na kuacha
kuwatumikisha watoto katika kazi ambazo hata kama wao ni masikini kiasi gani
sio vizuri kuwatumikisha kama wanyama. Suala la misingi hapa ni watu wote
katika jamii tuwe na hofu ya Mungu na vilevile tujiulize maswali, kwa mfano hao
watoto tunaowatumikisha kwa kazi ngumu je ndio wangekuwa ni watoto wetu
wanatumikishwa hivyo tungejisikiaje? Tuamini tusivyotaka watoto wetu watendewe
haipendezi kuwatendea watoto wengine hata kama hali zao ni ngumu kiuchumi na
hata wale waliotelekezwa.
TUWAJALI, TUWAPENDE NA TUWAEPESHE WATOTO NA AJIRA
NGUMU.
Comments
Post a Comment