TULITAFAKARI HILI
      Ni Watoto wa Mitaani sawa, lakini Vipaji vyao vyaweza kuleta Manufaa au Kuangamiza Taifa hili   (1500)  Views            Ukipita katika viunga vya miji mikubwa ya Tanzania, kuanzia Dar es  Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma, Morogoro na kadhalika, hushangai  kukuta watoto wakizurura mitaani huku wakati wa usiku wakiwa wamejilaza  katika vibaraza vya maduka na katika maeneo ya wazi kama kwenye viwanja  vya michezo. Kwao mvua ni yao, baridi ni yao na jua pia ni lao.     Watoto hao wanaishi katika mazingira hatarishi yanayowaweka katika  vishawishi vya kufanya uhalifu, kama vile uporaji na kujihusisha na  matumizi ya dawa za kulevya pamoja na biashara nyigine yoyote ile  haramu.      Katika hali ya kukosa chakula, malazi na mavazi kama mahitaji muhimu ya  mwanadamu, watoto hawa wamekuwa wakisukumwa kujihusisha na vitendo vya  kihalifu kama njia ya kujipatia riziki.     Wanapokuwa katika mazingira hayo, wanaweza kuja kuwa watu hatari na  tishio kwa taifa hili, hivyo kuigeukia ...