NI JUKUMU LETU SOTE KUFANIKISHA ELIMU JUMUISHI
MWANZONI mwa mwaka 2009, mke wa Rais, Salma Kikwete aliitaka jamii kutowatenga wanafunzi wenye ulemavu badala yake wasaidiwe na kushirikishwa katika masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo kupewa elimu kama ilivyo kwa makundi mengine ya kijamii. Siku aliyotoa wito huo hakusita kusema kuwa zaidi ya Sh milioni 881 zinahitajika kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kusomea kwa wanafuzi 8700 wenye ulemavu nchini ili waweze kujifunza katika hali mazingira mazuri. Tunapozungumzia mazingira mazuri kwa wanafunzi wenye ulemavu hatumaanishi vifaa na mahitaji mengine ya kitaaluma pekee bali hata miundombinu kama vyumba vya madarasa, vyoo, maktaba, maabara, mabweni na mazingira ya eneo zima la shule Kufanya hivi ni kuwapa fursa ya wao kujiona kuwa ni sehemu ya jamii hali itakayowapa ari ya kujifunza sambamba na wenzao wasiokuwa na ulemavu. Hili ni wazo zuri sana na naaunga na wewe Mama Salma KIkwete ila wazo hili mpaka kufikia leo 2015 halijafanikiwa kwa kiasi ki...