KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALEMAVU KITAIFA IRINGA , SERIKALI YA TANZANIA YAPIGA MARUFUKU UJENZI WA MAJENGO YASIYO RAFIKI NA WALEMAVU.
SERIKALI imeziagiza mamlaka za usafiri wa majini na nchi kavu (SUMATRA ) nchini kuanza mchakato wa kukaa na wamiliki wa vyombo hivyo ili kuanza uangizaji wa vyombo vya usafiri yakiwemo mabasi ambayo ni rafiki na walemavu nchini huku ikipiga marufuku majengo ya serikali kujengwa bila kuwepo kwa mchoro unaoonyesha mazingira yanayozingatia makundi yote ya jamii likiwemo la walemavu wa viungo . Agizo hilo limetolewa na waziri mkuu Mizengo Pinda wakati wa maadhimisho ya siku ya walemavu duniani yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya kichangani mkoani Iringa jana. Akiwahutubia walemavu hao na wananchi waliofika katika viwanja hivyo waziri mkuu ,aliyewakilishwa na waziri wa nchi ofi...