TANZANIA: MAISHA YA HATARI YA WATOTO WACHIMBA DHAHABU
Vijana wadogo wakike na wakiume wa Kitanzania wanashawishika kujiingiza katika uchimbaji wa dhahabu wakitumaini kupata maisha bora, lakini baadae wanajikuta wamekwama katika mzunguko mbaya wAa hatari na kukata tamaa. Tanzania na wahisani wanahitaji kuwatoa watoto hawa katika migodi na kuwaingiza shuleni au katika mafunzo ya ufundi stadi. Janine Morna, mtafiti wa haki za watoto wa shirika la Human Rights Watch (Dar Es Salaam) – Watoto wenye umri mdogo wa hadi miaka minane wanafanya kazi katika migodi midogo midogo ya dhahabu ya Tanzania, ikiwa na hatari kubwa kwa afya zao na hata maisha yao, shirika la Human Rights Watch imesema katika ripoti iliyotolewa leo. Serikali ya Tanzania inapaswa kukomesha ajira kwa watoto katika uchimbaji mdogo mdogo wa dhahabu, ikiwa ni pamoja na katika migodi isiyo rasmi, na isiyo na leseni, na Benki ya Dunia na nchi wahisani wanapaswa kuunga mkono juhudi hizi. Ripoti yenye kurasa 96, “Kazi ya Sulubu yenye Sumu: Ajira kwa Watoto na