UNYANYAPAA UNAVYOTUMIKA KUWANYIMA FURSA WATU WENYE ULEMAVU.
Na Francis ole Rikanga. TAFSIRI ya neno ulemavu hutofautiana kutoka kwa mtaalam moja hadi mwingine, kutokana na mazingira ambamo tafsiri hiyo hutumika. Baadhi ya wataalam hutafsiri kuwa ulemavu ni ukosefu wa viungo muhimu katika mwili wa binadamu na wengine husema ulemavu ni ukosevu wa fikra. Pamoja na watalaam na watu mbalimbali katika jamii kutofautiana, Bw.Fredy Msigallah ambaye ni Afisa mtetezi wa Haki za watu wenye Ulemavu kutoka CCBRT anasema ulemavu ni kukosekana au kuwepo kwa ukomo fursa ya kushiriki katika maisha ya kijamii kwa kiwango sawa na watu wengine kwa sababu za kimaumbile, kiakili na kijamii. Kwakwe ulemavu si ukosefu wa viungo bali ni ukosefu wa fursa ya kushiriki katika maisha ya jamii kunakosababishwa na vikwazo vya mazingira, kimtizamo na mfumo uliopo ndani ya jamii. Ni ukweli usiopingika kuwa licha ya kuwepo kwa vikwazo bado kuna watu wenye ulemavu waliodhihirisha kuwa ulemavu sio viungo. Ipo mifano hai ya watu wenye ulemavu iwe ya viungo, kuona...