SIKU YA MTOTO WA AFRIKA
Siku ya Mtoto wa Afrika na Elimu bora isiyo vikwazo Mtoto akitafakari Juni 16 ya kila mwaka Umoja wa Afrika sambamba na washirika wake husherekea siku ya mtoto wa Afrika- au kwa kimombo Day of African Child (DAC ), ikiwa ni kumbukumbu ya mwaka 1976 ambapo waandamanaji wanafunzi wa shule za Soweto Afrika ya Kusini waliandamana kupinga elimu iliyokuwa inatolewa kwa manufaa ya utawala wa kibaguzi wa makaburu. Maandamano hayo yalipokelewa na mikono usio na huruma na masikio yasiyo sikivu ya utawala wa kibaguzi na kusababisha vifo vya mamia ya wanafunzi “Watu wangu, leo nipo huru nipo huru kwa kuwa sintosahaulika kabisa, siku itatimia ambapo kila mmoja wetu atakuwa huru, huru kutokana na unyanyasaji, huru kutokana na uwoga, huru kutokana na kuuwawa, nyinyi ni vijana wadogo mtaishi hadi kuiona siku hiyo na ata kama sintofanikiwa kuiona siku hiyo nyinyi mnatakiwa kusadiki tu kuwa nitakuwepo siku hiyo, hapa ni nyumbani kwangu, pahala pangu pa kuishi.” Hayo ni