ONGEZEKO LA WATOTO WA MITAANI NA OMBAOMBA
IDADI kubwa ya watoto wadogo wanaoishi katika mazingira hatarishi inaweza kutishia amani nchini, ikiwa hatua za makusudi hazitachukuliwa kuokoa kizazi hicho. Hayo yalielezwa jana na Mkurugenzi wa Mradi wa Tuwalee FHI 360, Levina Kikoyo mara baada ya kufanyika kwa uzinduzi wa ripoti iliyofadhiliwa na Shirika la Misaada na Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID) ya utafiti uliofanyika kuanzia Februari mwaka huu juu ya kasi ya ongezeko la watoto hao. Alisema kwa sasa taifa lina watoto wengi walio katika mazingira hatarishi kutokana na kutopata elimu na kusababisha pia ongezeko la watoto hao mitaani, hali itakayozaa wimbi la ujambazi na uhalifu nchini katika siku za mbele. Alieleza kuwa kwa sasa zaidi ya watoto milioni 2 wanaishi katika mazingira hatarishi na hata wengine kujihusisha na shughuli za kuomba mitaani, na hivyo kuzua hofu ya matokeo mabaya kwa taifa. Alisema utafiti wao waliofanya katika wilaya zote tatu za Mkoa wa Dar e...