UENEZWAJI WA TAARIFA ZA ULEMAVUNI HATUA MUHIMU KWA JAMII DHIDI YA WALEMAVU..
Matukio katika ziara ya mtandao wa Thehabari.com kuangalia huduma za msingi kwa watu wenye ulemavu na uenezwaji wa taarifa juu ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Walemavu wilayani Arumeru kwa ufadhili wa ICD

Kikundi
cha Wanapambazuko Klabu cha Shule ya Msingi Iliboru wilayani Arumeru,
kikiwa katika picha ya pamoja. Kikundi hichi hufanya hamasa na
kuelimisha jamii juu ya haki anuai za watoto wenye ulemavu eneo hilo
ikiwa ni juhudi za ICD.

Bi.
Vick Kimaro ambaye ni mmoja wa viongozi wawakilishi wa watu wenye
ulemavu wilayani Arumeru, akionesha nakala ya chapisho lililoandaliwa na
Kituo cha Habari Kuhusu Ulemavu linalounadi Mkataba wa Kimataifa wa
Haki za Watu wenye Ulemavu alipozungumza na mwandishi wa mtandao huu
(hayupo pichani).

Mwalimu
Mkuu wa Kituo cha Wanafunzi wenye Ulemavu, Shule ya Msingi Naurei
wilayani Arumeru, Tuzie Mtenga akizungumza na mtandao wa Thehabari.com
kufafanua shughuli anuai za kituo hicho juzi
Mwalimu
Mratibu wa Kituo cha Walemavu cha Shule ya Msingi Iliboru, Loitusho
Yamat akifafanua jambo kwenye mahojiano na mtandao wa Thehabari.com jana
wilayani Arumeru
Baadhi ya wanafunzi wa darasa la nne (viziwi) katika Kituo cha Walemavu cha Shule ya Msingi Iliboru wakiandika darasani

Mwanafunzi
Richard Kisanga (18) wa Kituo cha Walemavu cha Shule ya Msingi Naurei
ya wilayani Arumeru akinakili hesabu kama alivyopewa maelekezo na
mwalimu wake
Baadhi
ya walimu waliopo katika mafunzo ya vitendo katika Kituo cha Walemavu
cha Shule ya Msingi Iliboru wakifundisha darasa la saba
Mmoja
wa wanafunzi wenye ulemavu (kiziwi), Shule ya Msingi Iliboru akiandika
darasani kama alivyokutwa na mpiga picha wa Thehabari.com
Comments
Post a Comment