TULITAFAKARI HILI
Ni Watoto wa Mitaani sawa, lakini Vipaji vyao vyaweza kuleta Manufaa au Kuangamiza Taifa hili (1500) Views Ukipita katika viunga vya miji mikubwa ya Tanzania, kuanzia Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma, Morogoro na kadhalika, hushangai kukuta watoto wakizurura mitaani huku wakati wa usiku wakiwa wamejilaza katika vibaraza vya maduka na katika maeneo ya wazi kama kwenye viwanja vya michezo. Kwao mvua ni yao, baridi ni yao na jua pia ni lao. Watoto hao wanaishi katika mazingira hatarishi yanayowaweka katika vishawishi vya kufanya uhalifu, kama vile uporaji na kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na biashara nyigine yoyote ile haramu. Katika hali ya kukosa chakula, malazi na mavazi kama mahitaji muhimu ya mwanadamu, watoto hawa wamekuwa wakisukumwa kujihusisha na vitendo vya kihalifu kama njia ya kujipatia riziki. Wanapokuwa katika mazingira hayo, wanaweza kuja kuwa watu hatari na tishio kwa taifa hili, hivyo kuigeukia ...