HILI NI LA KUANGALIA KWA JICHO LA PEKEE....
Tanzania ina shule moja tu ya sekondari ya viziwi! Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Elimu Maalumu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufindi Estrida Kimweri akieleza changamoto ya kuwa na shule moja ya sekondari kwa walemavu viziwi. Tanzania inakabiliwa na changamoto ya kuwa na shule moja ya sekondari kwa walemavu wasiosikia, toka ipate uhuru, hii haiendani na sheria ya mwaka 2010 ya walemavu ambayo inatetea kundi hilo kupata elimu. Akizungumza katika mahojiano maalum na Taarifanews.com Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Elimu Maalumu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Estrida Kimweri, changamoto hiyo inapelekea kukosa idadi kubwa ya walemavu wa aina hiyo wanaomaliza mpaka shule ya sekondari. Kimweri alisema kuwa shule hiyo ipo mkoa wa Njombe na kuna wanafunzi wengi sana wanaoletwa kutoka katika shule mbalimbali, kupata elimu ya sekondari kwenye shule hiyo, lakini nafasi yake ni ndogo sana kuweza kupokea wanafunzi wengi. Kwa sas...