MFANO WA KUIGWA NA WENGINE WENYE NAFASI YA KUISAIDIA HII JAMII,, NI JUKUMU LETU SOTE.
  GOLA KUWAONDOA WATOTO WA MITAANI JIJINI ARUSHA       Afisa  ustawi wa jamii na Maendeleo ya jamii jijini Arusha  Mwantumu  Dossi akitembelea mradi wa shamba la mahindi unaoendeshwa na taasisi ya  Gola Foundation jana katika kituo cha Kufikia watoto wa mitaani,katikati  ni Mkurugenzi wa shirika hilo  Elisha Maghembe habari picha  na l ibeneke la kaskazini blog    Mkurugenzi wa shirika lisilokua la kiserikali la Gola Foundation Elisha  Maghembe amesema kuwa wameanza zoezi la kuwaondoa watoto wa mitaani  walioko jijini Arusha na kuwafikisha kwenye vituo maalumu vya malezi  lengo ikiwa ni kuwarudisha makwao pamoja na kuwapatia fursa ya elimu  waliyoikosa kwa muda mrefu.     Elisha alisema kuwa zoezi hilo limeanza mapema mwaka huu ambapo mpaka  sasa wamewakusanya watoto 25 na kuwapeleka katika kituo chao cha malezi  kilichopo wilaya ya Arumeru ambapo watoto watano walitambuliwa na  kuchukuliwa na wazazi wao.     Amesema kuwa watoto wa mitaani wanapokaa mtaani kwa muda m...