UJUMBE WA SIKU YA WALEMAVU DUNIANI.
Ikiwa zimebaki takribani siku saba kabla ya kuadhimisha siku ya walemavu Duniani, kuna maswali mengi ya kujiuliza kama jamii tunayozungukwa na watoto pamoja na watu wazima wenye ulemavu wa aina tofauti tofauti, moja ya maswali hayo ni kama ifuatavyo, umeifanyia nini jamii ya watu wenye ulemavu,? umeguswa kwa namna gani na hali zao,? umekuwa ni mtu unaezidi kupotosha ukweli kuhusu ulemavu au ni mtu unayesaidia kuondoa mitazamo hasi dhidi ya watu wenye ulemavu? Je unawasaidia walemavu kwa kuwa unawahurumia au ni kwa sababu ni jukumu lako? sambamba na maswali mengine mengi na majibu tofauti tofauti, jambo moja la msingi ni kutathimini kwa kina ukuu na uweza wa Mungu kwa kila jambo, tofauti zetu zisitufanye tukadharauliana nakutokuthaminiana. Jambo la msingi tunapokaribia kuadhimisha siku ya walemavu Tanzania, ni kuhakikisha tunakuwa na upendo kwa watu wenye ulemavu tukiwachukulia ni sehemu muhimu ya jamii yetu, tushirikiane nao katika mambo mablimbali ya kijamii na kiuchumi kwa k...