ASILIMIA 90 YA WATOTO WALEMAVU HAWAENDI SHULE KUTOKANA NA DHANA POTOFU KATIKA JAMII MIMI NA WEWE TUSAIDIANE KUWATETEA WALEMAVU
 Serikali  imeombwa kulipa kipaumbele suala la umuhimu wa makundi ya walemavu  kupewa haki zao za msingi ikiwemo elimu kufuatia utafiti uliofanywa na  wataalama wa kimataifa wanaohudumia walemavu wa aina tofauti nchini  kubaini kuwa asilimia 98% ya makundi ya watoto wenye ulemavu hawaendi  shule kwa sababu mbali mbali ikiwemo dhana potofu iliyopo miongoni mwa  jamii.       Akizungumza  na mamia ya wananchi katika kijiji cha Duga kilichopo kata ya Duga  wilayani Mkinga katika zoezi la kuhamisisha jamii kuwapatia haki zao za  msingi walemavu  mtaalam wa kuhudumia walemavu kutoka nchini Thailand  Dr,Kirsi Salo  amesema katika utafiti wao walioufanya katika mikoa mbali  mbali nchini baadhi yao wamefichwa majumbani kutokana na imani haba za  kishirikina  kuwa kuzaa mtoto mlemavu ni mikosi ndani ya familia na  baadhi ya familia hudiriki hata kupoteza maisha yao.     Kwa  upande wake kiongozi wa kanisa la kilutheri usharika wa Duga mchungaji  Clementi Hongele ambaye amedai ...