MHESHIMIWA ANGELLAH KAIRUKI ATOA MSAADA WA BAISKELI KWA WOTOTO WENYE ULEMAVU WA VIUNGO.
Mheshimiwa
 akifafanua jambo kuhusu umuhimu wa kuwajali watoto wenye ulemavu kwa 
wazazi (hawapo pichani) waliofika kupokea msaada wa baiskeli kwa ajili 
ya watoto wao. Aidha, katika maelezo yake Mhe. Kairuki aliwasihi wazazi 
kutowaficha ndani watoto walemavu, bali wawapeleke shule na kuwapatia 
huduma zingine za muhimu ambaza wao kama binadamu wanatakiwa kuzipata. 
Pia aliwaomba wadau wengine wajitokeze kuwasaidia watoto wenye ulemavu 
kwani ni ndugu zetu na wanastajili kusaidiwa. Mheshimiwa Kairuki alitoa 
jumla ya baiskeli 35 kwa watoto wenye ulemavu wa Kawe, jijini Dar es 
Salaam
Mheshimiwa
 Kairuki akimkabidhi baiskeli na vifaa mbalimbali mtoto mmojawapo (jina 
halikufahamika mara moja) ambaye ni mlemavu wa viungo ili imsaidie 
wakati wa kwenda shuleni na mahali pengine.
Mheshimiwa
 Kairuki akimsikiliza Bi. Blandina Sembu ambaye ni Mratibu wa Shirikisho
 la Vyama vya Walemavu Tanzania (SHIVYAWATA) alipokuwa akitoa shukrani 
zake kwa Mhe. Kairuki baada ya kukabidhiwa baiskeli 35 kwa ajili ya 
watoto wenye ulemavu wa viungo katika Kata ya Kawe.
 Mmojawapo
 wa wazazi wa Kata ya Kawe akimshukuru Mhe. Kairuki (hayupo pichani) kwa
 niaba ya wazazi wenzake kwa moyo wake wa utoaji na wa kuwajali watoto 
wenye ulemavu na kuwapatia baiskeli zitakazowasaidia kufika shuleni na 
mahali pengine kwa urahisi.
Baadhi
 ya watoto wenye ulemavu waliofika kupokea baiskeli hizo kama msaada 
uliotolewa na Mheshimiwa Kairuki katika harakati zake za kuwasaidia 
watoto wenye ulemavu. 
Comments
Post a Comment