DISABILITY IS NOT INABILITY
WATOTO
WENYE MAHITAJI MAALUMU NA WANAOISHI KATIKA
MAZINGIRA MAGUMU NA VIPAJI TOFAUTI.
Mungu ana namna yake ya kipekee ambayo huitumia
kuonyesha ukuu wake katika ulimwengu. Mara nyingi binadamu huwa tunamkufuru
Mungu bila kuelewa uthamani wetu kwake. Kuna kila haja ya sisi wanadamu
kumrejea Mungu na kumuuliza ipi talanta yetu na njia ya kufanikisha ili kumpa
yeye utukufu. Inafika mahali mtu unayaishi maisha yako na unaona kabisa kuwa
yanaelekea ukingoni (unazeeka) bila kujua aliitumia vipi talanta yake katika
maisha yake na ni wangapi wamefanikiwa k upitia yeye, hii ni hatari sana kwa
maisha ya kiroho (life-after -life), pia ni hatari katika maendeleo ya kijamii.
Watoto wenye mahitaji maalumu, hasa wale wenye ulemavu
wana vipaji vingi ndani yao ijapokuwa inakuwa ngumu sana kwao kuvigundua. Kukosekana
kwa moja kati ya viungo vyao ama kiungo kutofanya kazi ipasavyo ikumbukwe kuwa
ni chachu ya viungo vingine kufanya kazi ipasavyo (unisensory-one sense the
better) hivyo kujikuta wakigubikwa na vipaji vya aina mbalimbali kama kuimba,
kucheza mpira, ku dansi, kuogelea na vingine vingi.
Hear My Voice imegundua pia watoto wanaoishi kwenye
mazingira magumu hasa watoto wa mitaani kuwa wana vipaji mbalimbali ambapo kama
wakiendelezwa kwa namna yoyote kifedha ama muongozo wa kimawazo wanaweza
kubadili maisha yao ya mitaani kupitia vipaji walivyonavyo na kujipatia
mahitaji yao muhimu kama shule, chakula na mavazi.
Kwa kutambua haya,team nzima ya Hear My Voice imezindua mission mpya ya
kugundua, kutafuta na kuendeleza vipaji vya watoto wenye ulemavu na watoto
wanaoishi katika mazingira magumu kwa malengo ya kuwafanya waweze kujitegemea
katika maisha yao na kutokuwa ombaomba na watu wasiothaminika katika jamii.
(DISABILITY IS NOT INABILITY), they can change their
handicap world and be great people in the world. Watu kama Hellen Keller, Lenna
Maria, Voice Wonder, Keisher, Mabaga fresh na Fox Brown ni mfano wa walemavu
wenye mafanikio huku wengi wao wakitumia vipaji vyao kuionyesha dunia kuwa
ulemavu sio mwisho (limit) ya kufanya kitu, they can do many things in
different ways, only and only if we are together to recorgnize what they are
capable of, that’s why Hear My Voice inaomba jamii kwa ujumla kutoa ushirikiano
juu ya hili, kuwatambua na kuwaendeleza watoto wenye vipaji.
Disability
is a matter of perception; if you can do just one thing well, you are needed by
someone. “Martina Nauratilova”
Comments
Post a Comment